Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Books
  • Publish
  • Sell
  • Courses
  • Blog
  • Support
  • Sign in
  • All books
  • Discounts
  • Swahili books
    • Afya na ustawi
    • Dini
    • Fasihi
    • Malezi
    • Ndoa na mahusiano
    • Maendeleo binafsi
    • Uchumi na biashara
    • Uongozi na usimamizi
    • Vitabu vya kiada
  • English books
    • Business and finance
    • Health and wellness
    • Literature
    • Parenting and relationships
    • Personal development
    • Religion and spirituality
    • Textbooks
  • Children's books
  • Online courses
  • Free books
  • Books
  • Swahili books
  • Dini
  • Kukaa Kwenye Nafasi Yako

Kukaa Kwenye Nafasi Yako

  10,000.00 TZS
Add to cart
Downloadable file How to buy

Nafasi ni mahali ambapo Mungu humuweka mtu ili aweze kumfanikisha kwa mafanikio ya rohoni na mwilini. Ni mahali ambapo Mungu akitaka kukutana na wewe anakuja hapo. Mtu anapokuwa nje ya nafasi ni wazi kuwa anapishana na mambo mengi sana ambayo Mungu anakuwa ameyakusudia katika wakati husika. Hakuna kilicho bora kutoka kwa Mungu kinachoweza kuendelea katika maisha ya mwanadamu akiwa nje ya nafasi.

Kila nafasi ina marupurupu yake. Kinachoamua mtu kuendelea kupokea au kusitishiwa marupurupu ni nafasi. Kiongozi yeyote anapoondolewa kwenye nafasi au anapopoteza nafasi aliyokuwa nayo moja kwa moja viambata vya ile nafasi huondolewa kwake. Vile viambata vya nafasi aliyokuwa nayo haviondolewi kwake kwa sababu hapendwi, la hasha!

Vinaondolewa kwake kwa sababu anakuwa hana kigezo kikuu tena. Mtu kukaa kwenye nafasi yake ndio kigezo kikuu cha kufanikishwa na Mungu. Inawezekanaje udai mshahara wa meneja wakati wewe ni mwalimu? Mshahara huamriwa na nafasi. Kwa hiyo ukiutaka mshahara wa meneja, basi unatafuta kwanza nafasi ya umeneja, mshahara utakufuata wenyewe.

Ndio maana ikiwa unamwamini Mungu na unaona mambo hayaendi sawa, angalia ikiwa umekaa kwenye nafasi au la! Ni kosa kufikiri Mungu hakupendi ikiwa mambo yanakuendea vibaya.

Upendo wa Mungu kwako sio kigezo cha kwenda nacho kwenye maombi wakati unapotaka Mungu akufanikishe. Upendo wa Mungu kwako sio mbadala wa kukaa kwenye nafasi. Mungu anaweza kuwa anakupenda vizuri tu lakini ili akutane na wewe na kuthibitisha upendo wake kwako ni lazima akukute kwenye nafasi. Suala la kupoteza nafasi ni la kiroho kwanza kabla ya kuwa la kimwili.


Others Also Bought

Chochea Kipaji Chako
Chochea Kipaji Chako
5,000.00 TZS 4,500.00 TZS
HILI NI NENO LA KUFAA KWAKO - Siku 21 za kukua, kujijenga na kujiimarisha kiroho
HILI NI NENO LA KUFAA KWAKO - Siku 21 za kukua, kujijenga na kujiimarisha kiroho
9,999.00 TZS 7,500.00 TZS
Stay in Your Position
Stay in Your Position
10,000.00 TZS

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Books
  • About us
  • Publish
  • Sell
  • Blog
  • Support
  • Sign in
DL Bookstore © 2026. All rights reserved | Made with ❤️ in Tanzania.