Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Mafundisho awali ya Neno la Mungu
Kupitia kitabu hiki utajifunza masomo ya awali ya Biblia na ya msingi ya wokovu. Masomo hayo ni: Wokovu , Ubatizo wa Kikristo, Ubatizo wa Roho Mtakatifu, Biblia, Maombi, Kusifu na kuabudu, Majaribu, Vita vya kiroho na kutumia mamlaka , Utoaji, Kushuhudia/Uinjilisti, Mambo ya siku za Mwisho na Imani potofu.
Kila Mkristo anaweza na anapaswa kufahamu Biblia na mafundisho ya msingi ya Kikristo. Wakristo wengi wanadhani wanajua Biblia vya kutosha. Ujinga hauna faida na ujinga wa makusudi ni dhambi.
Baada ya kumaliza kujifunza masomo haya utaweza kumtumikia Mungu kwa ufanisi katika huduma mbalimbali kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo (Kanisa) na kutimiza kusudi lake la ki-Mungu na wito wake.Pia utaboresha uwezo wako wa kuyaelewa maandiko, kuyatafsri na ujuzi wako katika kuhubiri.
Kusudi kubwa ni kubadilisha maisha ya watu yawe bora zaidi kwa kuyaelewa katika vitendo masomo yote utakayojifunza ili uweze kutumia maarifa na ujuzi.
Mungu akubariki sana