SI KUTUMIKA TU, BALI KUIDHINISHWA
Katika kipindi ambacho huduma nyingi zinatawaliwa na umaarufu, vipawa, na mafanikio ya nje, ujumbe wa kweli kuhusu kibali cha Mungu umepotea katika kelele za umaarufu wa wanadamu. Kitabu hiki kinaleta mwanga mpya juu ya tofauti kati ya kutumika na kuidhinishwa, kikiweka wazi kuwa si kila anayehudumu amepitishwa na Mungu, na si kila aliyepata jukwaa ana kibali cha mbinguni.
Kupitia sura kumi zenye ufunuo na ushuhuda wa maandiko, nimeeleza kwa kina kuhusu,
- Tofauti kubwa kati ya kutumika kwa sababu ya vipawa na kutumika kwa sababu ya kibali.
- Hatari ya kujenga huduma kwa misingi ya sifa badala ya uthibitisho wa Mungu.
- Ishara za mtumishi aliyeidhinishwa na aliyepitishwa na Mungu.
- Namna ya kupita mitihani ya kiroho kuelekea kuidhinishwa.
- Siri za huduma inayodumu na kuzaa matunda ya milele.
Hiki si kitabu tu cha mafundisho, bali ni mwongozo wa mabadiliko ya kiroho kwa kila anayetamani kutumika kwa namna inayompendeza Mungu. Ni mwaliko wa kurudi kwenye msingi wa huduma yenye mizizi ya unyenyekevu, utiifu, na kibali halisi kutoka kwa Baba.
Kama unataka si kutumika tu bali kuwa na alama ya kupitishwa na Mungu, basi kitabu hiki ni kwa ajili yako.
Recommended for you
