Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Books
  • Publish
  • Sell
  • Courses
  • Blog
  • Support
  • All books
  • Discounts
  • Swahili books
    • Dini
    • Fasihi
    • Maendeleo binafsi
    • Malezi
    • Ndoa na mahusiano
    • Uchumi na biashara
    • Uongozi na usimamizi
    • Vitabu vya kiada
  • English books
    • Business and finance
    • Literature
    • Parenting and relationships
    • Personal development
    • Religion and spirituality
    • Textbooks
  • Children's books
  • Online courses
  • Free books
  • Books
  • Swahili books
  • Dini
  • Tamaa na Shauku Vinavyoathiri maisha ya mtu

Tamaa na Shauku Vinavyoathiri maisha ya mtu

8,000 TZS  4,000 TZS
Add to cart  

Ndani ya kila mwanadamu, kuna nguvu mbili zinazofanana kwa nje lakini zina matokeo tofauti kabisa, yaani Tamaa ja Shauku. Neno moja huweza kumvuta mtu kwenye anguko la milele, na jingine linaweza kumuinua mtu hadi kwenye kusudi la Mungu katika maisha yake. Hizi ndizo nguvu ambazo kitabu hiki kimejikita kuzichambua kwa undani wa kiroho na kimaandiko. 

Katika dunia ya sasa iliyojaa vishawishi, mitazamo ya kibinadamu, na misukumo ya kimwili, ni rahisi kwa mtu kuchanganya tamaa na shauku. 

Wengi wameharibu maisha yao wakidhani wanatafuta maendeleo au mafanikio, kumbe walikuwa wanatawaliwa na tamaa ya mwili isiyoweza kudhibitiwa kwa akili na ujanja wa mwanadamu. Wengine wamezimisha shauku halali ambayo Mungu aliweka ndani yao kwa sababu waliambiwa kuwa ni tamaa mbaya, matokeo yake wakajikuta wakiishi chini ya kiwango cha kiungu. 

Kitabu hiki si tu cha mafundisho, bali ni taa ya kiroho ya kuelekeza njia kati ya mambo haya mawili, yaani Tamaa na Shauku. 

Kwa msaada wa maandiko matakatifu, mifano ya maisha halisi, na ufunuo wa kiroho, nimejitahidi sana kueleza Tofauti iliyopo kati ya Tamaa ja Shauku, Madhara ya Tamaa katika maisha ya mtu, Uzuri na nguvu ya Shauku Takatifu, Jinsi ya kuijua Tamaa iliyojificha ndani yako, Njia ya kutakaswa, kusawazishwa na kuelekezwa kwa usahihi. 

Kitabu hiki ni kioo cha moyo wa mtu. Ukikisoma kwa unyenyekevu, utagundua ni nini kinaleta vikwazo katika maisha yako, na pia utapata njia ya kuachilia kile ambacho Mungu amekuwekea kama shauku halali inayolenga kuchochea utukufu wake. 

Tamaa huharibu hatima. Shauku huendeleza kusudi. Chagua kusoma, kutafakari na mruhusu Roho Mtakatifu azungungumze nawe.


Others Also Bought

Usikate Tamaa, Lipo Tumaini
Usikate Tamaa, Lipo Tumaini
7,000 TZS
Chochea Kipaji Chako
Chochea Kipaji Chako
5,000 TZS 4,500 TZS
Lishinde Jaribu
Lishinde Jaribu
5,000 TZS

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Books
  • About us
  • Publish
  • Sell
  • Blog
  • Support
DL Bookstore © 2026. All rights reserved. | login