UKUZAJI WA KANISA LILILO IMARA (kwa tafsiri ya mifano ya Yesu – kwa matumizi ya watu wa siku hizi)
Mifano aliyo itumia Bwana Yesu kufundishia imebeba kiini cha ujumbe jumla wa mbinguni. Kwa kujifunza maana ya mifano yote ya Yesu tunaweza kukua na kuimarika kiroho kwa kiwango cha kutoyumbishwa kwa elimu za uongo na mapito ya dunia. Mifano ya Yesu imejaa ujuzi wote wa kiroho unao mtoshereza mkristo kuishi sawa sawa na mapenzi yote ya Mungu yaliyoainishwa kupitia neno lake.
Kitabu hiki kinalenga kuhainisha maisha halisi ya mkristo mwaminifu yaliyo kusudiwa na Mungu kwa kumtuma mwanawe Yesu Kristo kuwa mwokozi wa ulimwengu. Ifuatayo ni baadhi ya mifano ambayo imefafanuliwa ili kuleta mwanga wa kiroho na ujuzi wa kweli za Mungu kwa wacha Mungu.
Others Also Bought
Mambo Muhimu kwa Mwalimu wa Biblia Unapoandaa Somo
Ifahamu Biblia Vizuri
TZS 10,000