Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Yesu Akawafundisha, Akisema Heri
Heri tisa (Mathayo 5:1-12), ni maneno aliyoyasema Bwana YESU mwenyewe. Kwa hiyo yana uzito mkubwa na yanastahili kuzingatiwa kwa umakini mkubwa na kila muumini. Leo hii, mimi na wewe (kama waumini wake), ndiyo walengwa wa Bwana Yesu.
Tumepokea kijiti kutoka kwa Mitume wa Bwana Yesu. Kwa hiyo tutafakari mafundisho haya kwa makini; kwani ni nyenzo za kuhubiri Injili. Heri hizi zikakupe kutafakari na kujifanyia tathmini maishani mwako ili uweze kuona ni wapi panahitaji marekebisho, na kwa msaada wa Bwana utavuka na kutoka na ushindi mkuu sana. Yesu akilisema jambo basi ujue anategemea nasi tulibebe katika uzito ule ambao nae ameona tunapaswa kulichukulia.
Kufanikiwa ki-Mungu inawezekana. Kuinuka ki-Mungu inawezekana, ni swala la kuzifahamu kanuni na kuziweka katika matendo bila kuyumbishwa na mazingira yoyote yale.