Karantini
Pata picha ukiwa ndani ya jengo, umefungiwa na kundi kubwa la watu kwa zaidi ya mwaka mzima, ukiukosa uhuru wako wa kutoka nje na kufanya shughuli zako za kila siku kama watu wengine, umefungiwa mithili ya mfungwa ijapokuwa si mfungwa na mahala ulipo si gerezani, ukiwa huujui usiku wala mchana kwa maana sehemu uliyowekwa ni chini ya ardhi mfano wa handaki na hakuna madirisha ya kukuwezesha kuona nje, kilichosaidia uweze kupata nuru na kuona ni mwanga mkali wa taa zilizowaka kwa saa ishirini na nne ili kuliepusha giza nene lililotanda wakati wote.
Yote tisa, kumi ni kwamba jengo hilo lilikuwa kama kuzimu iliyoshuka duniani kwani kila siku iendayo kwa Mungu watu uliofungiwa pamoja nao walikufa hovyo mithili ya kuku machinjioni, kila baada ya saa kadhaa maiti zilibebwa na kutolewa nje kwa ajili ya kuzikwa kwa mazishi ya pamoja (mass grave) ambayo hakuna ndugu wa marehemu hata mmoja aliyepata nafasi ya kuhudhulia, huku ndani ya jengo hilo kukiwa na msongamano mkubwa wa wagonjwa waliokuwa hoi bin taaban kwa maradhi ambayo walijua dhahiri kuwa kifo ndio hatima yake.
Others Also Bought