Kwanini najuta!
Kitabu cha “kwanini najuta” ni kitabu ambacho kina hadithi fupi fupi ambazo zinazungumzia masuala mbalimbali ya ukatili, unyanyasaji, dhuluma, uzalilishaji unaojitokeza katika maisha ya watu wazima, watoto na wanawake. Pia kitabu hiki kinatoa burudani na kukuza stadi za lugha ya Kiswahili kwa wasomaji wapya na wenyeji wa lugha hii.
Hadithi hizi zaweza kuwa na vionjo vya ukweli pia vionjo vya kutunga ili mradi tu ujumbe uliokusudiwa ufike kwa msomaji ili uweze kutoa mchango katika jamii na mwisho kujenga vizazi vyenye hofu ya kufanya ukatili, unyanyasaji,dhuluma,uzalilishaji miongoni mwa makundi ya watoto,wanawake,wanaume na wengine wenye nia mbaya. Ninaamini utakapo kisoma kitabu hiki,utapenda kukirudia mara kwa mara,kwani kina mambo muhimu yanayo igusa jamii moja kwa moja.
Mbali na kuigusa jamii moja kwa moja pia utatumia maarifa na ujuzi huo katika maisha yako ya kila siku, kwenye majukwaa mbali mbali ya kifamilia,kijamii kama mifano katika kuiasa jamii ili iwe na hofu ya kufanya maovu.
Pamoja na kupata ujuzi na maarifa mbalimbali katika kitabu hiki pia utaburudika vya kutosha na utakuwa balozi kwa kuwasimulia ndugu ,jamaa na marafiki ili nao waweze kujipatia nakala hii kwa manufaa yao na familia zao.
Others Also Bought

