Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support
  • All books
  • Offers
  • Swahili books
    • Dini
    • Fasihi
    • Maendeleo binafsi
    • Malezi
    • Ndoa na mahusiano
    • Uchumi na biashara
    • Uongozi na usimamizi
    • Vitabu vya kiada
  • English books
    • Business and finance
    • Literature
    • Parenting and relationships
    • Personal development
    • Religion and spirituality
    • Textbooks
  • Children's books
  • Online courses
  • Free books
  • Get books
  • Swahili books
  • Maendeleo binafsi
  • Heshima kwa Wazee kichocheo cha mafanikio

Heshima kwa Wazee kichocheo cha mafanikio

TZS 2,000

Paperback eBook
Add to cart  

Mafanikio; umekuwa msamiati pendwa kwa kila mmoja kutamani kufanikiwa na wengine wakienda mbali zaidi kwa kutamani mafanikio ya haraka kitu ambacho kimegharimu utu na maisha ya wengi, kwa upande mwingine mafanikio ni kitu kizuri cha kujivunia ikiwa kitatokea kwa kufuata utaratibu wa mafanikio.

Nduguyangu ni vyema ukatambua kuwa mafanikio hayatokei tu, mafanikio ni matokeo ya juhudi za kimakusudi za kufuata kanuni na taratibu za kufanikiwa, naweza kusema mafanikio ni mazao ya kufuata kanuni na taratibu za mafanikio. Kuna kanuni nyingi ambazo zinaweza kumsaidia mtu kufanikiwa katika chochote anachokusudia kufanikiwa mfano kitaaluma, kikazi, kibiashara, kifamilia n.k. Mojawapo ya kanuni hizo ni pamoja na kuwa na maono, kuweka malengo, nidhamu binafsi, kuwa na watu sahihi kwenye maisha, kuwa na heshima na mtazamo chanya n.k

Kwa mlengo wa kitabu hiki tunajikita katika kutambua siri moja ya mafanikio ambayo ni heshima na zaidi tutaangalia heshima kwa wazee wetu na namna ambavyo inaweza kimaalumu kabisa kumsaidia mtu kufanikiwa katika mambo mbalimbali ikiwepo kitaaluma, kiuchumi, kifamilia na kimaisha kwa ujumla

Ili kuzuia madhara ya kuwa na jamii isiyothamini wazee wala kuwaheshimu ambayo ni nidhamu na maadili kuzidi kuporomoka na mafanikio kubaki kuwa ndoto isiyotimia kwa wengi ni vizuri tukajifunza zaidi jambo hili.

Ukizingatia kuwa mafanikio ni ndoto ya kila mtu lakini ili ndoto hii iweze kutimia kuna namna ya mtu anatakiwa kuwa ili kuchochea mafanikio yake na mojawapo ya kichocheo hicho ni kutambua nafasi ya wazee na kuwapa heshima wanayostaili.

Kitabu hiki kimelenga kupanua uelewa wa mtu binafsi na jamii kuhusu heshima kwa wazee kwa kutambua ikiwa wazee wetu watapata heshima wanayostahili itakuwa vyepesi sana kuheshimu wakuu wetu wa kazi, wafanyakazi wenzetu, familia na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kufanikiwa.


Recommended for you

Funguo 7 za mafanikio kwa Mkristo
Funguo 7 za mafanikio kwa Mkristo
TZS 15,000
View options
Mafanikio Ni Haki Yako
Mafanikio Ni Haki Yako
TZS 4,999
View options
Misingi 10 ya Mafanikio Yako
Misingi 10 ya Mafanikio Yako
TZS 2,999
View options

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2025. All rights reserved.