Meditation (Tahajudi kwa Wanaoanza)
Katika kurasa za kitabu hiki, utapata maarifa ya msingi ya Tahajudi, mbinu za kuanza kwa urahisi, njia za kushinda vikwazo vya awali, na msukumo wa kukuongoza kuendelea na safari yako ya ndani bila kukata tamaa. Hakuna presha, hakuna mashindano, ni wewe na nafsi yako mkiwa na nafasi ya kujielewa zaidi.
Kuna wakati katika maisha yako unaweza kuhisi kuelemewa na kila kitu. Kelele za dunia zinaweza kukuzidi nguvu kuliko sauti ya ndani ya moyo wako. Unaweza kuwa unaonekana kuendelea mbele kwa nje, lakini ndani yako kuna huzuni, sintofahamu, na uchovu wa kiakili uliokithiri. Utajikuta ukitafuta maana ya maisha, utulivu wa kweli, na nafasi ya kupumua bila kuhisi mzigo wa dunia hii. Hapo dipo unapokutana na Tahajudi – kama mfariji mkuu.
Kazi ya Tahajudi sio kuzuia hayo yote yasitokee, bali kukupa nguvu na mtazamo mpya juu ya maisha.
Natumaini utasoma kitabu hiki kwa moyo mkunjufu, na zaidi ya yote, utajiruhusu kujaribu. Hata kama ni dakika moja tu kwa siku. Naamini kuwa ndani yako kuna utulivu mkubwa unaokusubiri. Kuna nuru ya ndani inayotamani kung’aa tena. Na kila wakati utakapokaa kimya, ukavuta pumzi na kusikiliza, utakuwa unakaribia zaidi kwenye hiyo nuru.
Hii si hadithi tu, bali ni mlango wa kukukaribisha katika safari ya ndani – safari ya kutambua kuwa amani na majibu yote yapo ndani yako.
Others Also Bought

