Mwongozo Halisi wa Mabadiliko Chanya
Kitabu hiki kikiwa ni toleo la pili ni mwongozo halisi na madhubuti kwa mtu yeyote mwenye shauku ya kuona maisha yake yanabadilika katika hali chanya.
Zipo kanuni, mbinu muhimu, misingi na hatua za kuzingatia, vitu vya kufanya na vya kuacha vingine vya kupunguza ili uone maisha yako katika huu mwaka yanabadilika jumla katika hali chanya na uwe na uhakika wa kesho njema.
Mabadiliko chanya yana mkondo wake maalumu kwa mtu aliyetayari na mwenye kiu na anauwezo wa kulipa gharama zinazotakiwa kuwa na mabadiliko chanya iwe katika ukuaji chanya katika Kiroho, Ujenzi wa fikra chanya na kuwa na mabadiliko chanya katika mwili na mambo mengine kiuchumi, kiafya n.k
Ndani ya kitabu nimeeleza, maana halisi ya mabadiliko, aina za mabadiliko chanya na hasi, mbinu za msingi kukuletea mabadiliko chanya, hatua za kufuata kukuletea mabadiliko chanya, mwongozo wa kujitathimini na mengine mengi.
Kikubwa unapaswa kufanyia kazi ujumbe huu ili iwe wakala wa mabadiliko chanya na mleta suluhulisho na usiwe mlalamikaji au mkimbia majukumu.
WAKALA WA MABADILIKO CHANYA
Recommended for you
