Sayansi ya kujizuia
Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye hatima yake ni ndogo. Kila mmoja Mungu amemuumbia hatima kubwa kwenye maeneo tofauti tofauti hapa duniani, lakini mfumo wa maisha yake ndo utaamua aifikie hatima hiyo kwa ukubwa gani (aidha mdogo au mkubwa au asiifikie kabisa)
Mfumo wa maisha ya mtu unahusishwa sana na hatima ya mtu kwasababu mtu mwenyewe pamoja na mfumo wake wa maisha upo hapa hapa ulimwenguni.
Na ukweli ni kwamba duniani sahivi pamejaa kila aina ya ajenda (nzuri na mbaya) ni wewe mwenyewe tu uchague ni ajenda zipi uzifuate na kuzifanya kuwa mfumo wako wa maisha na zipi uachane nazo kutegemeana na ile hatima unayo iendea.
Sasa KUJIZUIA kunafuata pale ambapo mtu anakutana na mambo mengi sana ya hapa duniani lakini anaamua kutokuyafanya yote ila anachagua yale kadhaa ambayo yana mchango kwenye kuifikia hatima yake kubwa (maono yake).
Ukweli ni kwamba hauwezi kuifikia hatima yako (kutimiza maono yako) kama wewe utakuwa unafanya kila kitu kinachokatiza mbele ya maisha yako, ni lazima mengine uyaache ili uwe salama wewe na kizazi chako, ndomana neno la Mungu kweye kitabu cha Mithali 29:18 linasema kwamba Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
Kutambua unapoelekea (maono yako) kuna faida kubwa sana kwa mtu ambaye kiu yake ni kuacha alama kwenye ulimwengu wa kizazi chake na wa vizazi vinavyo fuata baada yake. Kuyatambua maono msaada wake mkubwa ni kwamba, kuna mwezesha mtu kuchuja ni mambo gani ajihusishe nayo na mambo gani hatakiwi kujihusisha nayo [ Huku ndo kunaitwa KUJIZUIA]
Sasa hautajizuia kwa mabaya tu, kuna wakati utajizuia hata kwenye kufanya mambo mazuri ambayo wengine wanayafanya.
Recommended for you


