Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support
  • All books
  • Offers
  • Swahili books
    • Dini
    • Fasihi
    • Maendeleo binafsi
    • Malezi
    • Ndoa na mahusiano
    • Uchumi na biashara
    • Uongozi na usimamizi
    • Vitabu vya kiada
  • English books
    • Business and finance
    • Literature
    • Parenting and relationships
    • Personal development
    • Religion and spirituality
    • Textbooks
  • Children's books
  • Online courses
  • Free books
  • Get books
  • Swahili books
  • Maendeleo binafsi
  • Tambua majira na nyakati ili ufanikiwe

Tambua majira na nyakati ili ufanikiwe

TZS 9,500  TZS 4,000

Paperback eBook
Add to cart  

Katika safari ya maisha, kila mtu anakutana na nyakati tofauti za kupanda na kushuka, furaha na huzuni, kupokea na kusubiri. Hata hivyo, changamoto kubwa ambayo wengi wanakutana nayo ni kujua namna ya kutambua majira wanayopitia, na pia namna ya kujipanga kulingana na yale ambayo Mungu amepanga kwa wakati huo. Kitabu hiki, Tambua Majira na Nyakati ili Ufanikiwe, kimeandikwa kwa kusudi kuu la kumsaidia msomaji kugundua hekima ya Mungu kuhusu nyakati, na namna ya kuishi kwa ufanisi ndani ya kila majira.

Biblia inatufundisha wazi kuwa maisha yetu yamepangwa kwa majira tofauti. Kama inavyojulikana katika Mhubiri 3:1, “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.” Maandiko haya kutoka kitabu cha Mhubiri yanatufundisha kwamba hakuna jambo au tukio linalotokea kwa bahati mbaya. Kila jambo lina muda wake maalumu. Lakini swali ni: Je, tunalitambua hilo? Tunajua lini ni wakati wa kupanda, na lini ni wakati wa kuvuna? Lini ni wakati wa kusubiri, na lini wa kutenda?

Mafanikio halisi ya maisha haya yanategemea zaidi uwezo wa mtu kutambua kile Mungu anachofanya katika majira mbalimbali, na kujiweka sawasawa na hilo. Kupitia kitabu hiki, utajifunza jinsi ya kutambua nyakati za Mungu katika maisha yako,

Ni matumaini yangu kuwa kitabu hiki kitakuwa msaada mkubwa kwako, kukufungua macho ya kiroho, na kukuongoza katika njia ya mafanikio katika maisha yako. Mungu anataka usimame imara kila wakati, ukijua linapokuja giza au nuru, mvua au kiangazi, ukame au utele na kuishi kwa hekima inayotoka juu.

Karibu tujifunze pamoja.



Recommended for you

Funguo 7 za mafanikio kwa Mkristo
Funguo 7 za mafanikio kwa Mkristo
TZS 15,000
View options
Misingi 10 ya Mafanikio Yako
Misingi 10 ya Mafanikio Yako
TZS 2,999
View options
Mwongozo katika mafanikio
Mwongozo katika mafanikio
TZS 10,000
View options
Mafanikio Ni Haki Yako
Mafanikio Ni Haki Yako
TZS 4,999
View options

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2025. All rights reserved.