Uwe Hodari, Ujionyeshe kuwa Mwanaume.
Kitabu hiki kimefika wakati muafaka kabisa ambao dunia inahitaji zaidi wanaume watakaosimama katika nafasi zao Kwa uhodari, uimara na ushujaa.
Ukweli ni kwamba katika dunia ya leo wanaume hodàri ni wachache sana pamoja na uwepo wa maelfu ya watu wa jinsia ya kiume. Iko wazi kwamba unaweza kuwa mtu mzima pia wa kiume na bado usiwe mwanamume.
Kujionyesha kuwa mwanamume siyo tu kuvaa mavazi ya kiume, sauti nzito, maumbile ya kiume bali zaidi ni kusimama imara na kwa uhodari katika majukumu na nafasi ya mwanamume kama mhimili wa ujenzi wa familia, jamii, taasisi, taifa na ulimwengu ulio salama.
Ongezeko la maasi kama ushoga, ndoa za jinsia moja, uwepo wa jinsia zingine zaidi ya mwanamke na mwanamume imepelekea idadi ya wanaume hodari kuwa adimu kwa sasa ulimwenguni kote.
Ujumbe huu ni zawadi ya thamani mno kwako ili uweze kujua namna sahihi ya kujionyesha kuwa mwanamume.
Ndani ya kitabu hiki kuna mengi ya kujifunza kupitia wanaume waliojionyesha kuwa wanaume, maamuzi sahihi kwa mwanamume, majukumu na nafasi ya mwanamume katika ujenzi wa hatima bora ya ulimwengu.
Kitabu hiki kinapaswa kusomwa na kila mvulana, kijana wa kiume pamoja na mtu mzima wa jinsia ya kiume ili tupate watu watakao amua kujionyesha kuwa wanaume kweli kweli.
UWE HODÀRI UJIONYESHE KUWA MWANAUME.
Recommended for you
-9b18bee2.jpg?7147732)
