Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Wewe ni nani?
Kila mtu hapa duniani aliumbwa kwa kusudi fulani, kila mmoja kuna kazi alipewa kabla hajazaliwa ambayo anapaswa kuifanya kabla ya kifo chake. Kila mmoja ana sifa
fulani ya kipekee aliyoumbwa nayo ambayo katika hiyo Mungu hujidhihirisha katika ulimwengu huu na kujinyakulia utukufu.
Ndani yako kuna hazina kubwa iliyositirika, hazina ambayo ili kuijua lazima umjue kwanza aliyekupa hazina hiyo ambaye ni Mwenyezi Mungu. Hazina hiyo iliyopo ndani yako haipo kwa ajili ya faida yako wewe mwenyewe bali iliwekwa kwako ikawe faida kwa wengine, iliwekwa kwako ili kuongeza thamani katika maisha ya watu na dunia kwa ujumla.
Jambo la kusikitisha watu wengi tunaishi pasipo kutambua hazina hiyo matokeo yake hata wale waliowekwa karibu yetu ili hazina hiyo iwasaidie hawapati kitu.
Ni heri kutokuzaliwa kabisa kuliko kuishi au kufa bila kujua au kutimiza kusudi la mtu kuletwa duniani