Mambo 23 Yamfanyayo Mwanamke Ajute Kuolewa
Mwanamke hukerwa na mwanaume anaye mwingilia kimwili kabla ya kumwandaa, asiye shiriki hali yake ya ujauzito, “Anaye mteka nyara” ili kufisha kusudi la kuumbwa kwake, asiye shaurika, asiye na shukurani. (Mnung’unikaji), asiyetenga muda kwa ajili ya faragha pamoja naye, asiye mshirikisha katika huduma, anaye onyesha wazi wazi kuwajali wazazi wa upande wake, asiye mwangalia usoni na kumtamkia neno kuhusu urembo wake, anaye tumia madaraka ya ofisini nyumbani kwake, anaye onyesha hali ya kutojali mahitaji yake ya muhimu (Mahitaji ya kike) “Mzalilishaji” mwenye maneno na matendo ya unyanyasaji kijinsia, anayefanya mambo kwa upendeleo dhidi ya watoto wao waliowazaa pamoja, asiyejali hisia zake anapomtaka kwa ajili ya tendo la ndoa, anaye mtumia kama chombo tu cha kujiburudishia, anaye mfanya kuwa mtumwa wa kazi tu, anaye mnyima nafasi yake ya kutoa maamuzi katika familia, mkali, katili anayependa ugomvi, asiyetaka mkewe kumiliki chochote mikononi mwake, asiyeweza kumlinda dhidi ya mashambulizi, asiye mjali kwa kumtunza, mchafu asiye kubali kuoga wala kupiga mswaki, asiye mtoshereza kitandani.
Others Also Bought