Kiongozi Aliyefanikiwa
KUSUDI LA KITABU HIKI: kitabu hiki kimeandikwa kwa lengo la kumsaidia msomaji kukuuza uwezo wake wa kiuongozi ambapo kitabu hiki chaweza kutumiwa kufundishia viongozi mbalimbali ili kuwasaidia viongozi kuongoza kwa mafanikiao.
Nimeandika kitabu hiki huku nikiamani kuwa wewe unayesoma kitabu hiki na kukitumia ni kiongozi, ambapo naamini kuwa utakaposoma kitabu hiki na kukielewa vizuri kitakukuza na kukuongezea Zaidi uwezo na maarifa ya kiuongozi ambapo uongozi wako utakuwa ni wenye mafanikio makubwa sana. Ninao uhakika kabisa kuwa mawazo ya kiuongozi yaliyo andikwa ndani ya kitabu hiki ni mazuri na yenye hakika zenye kukuwezesha katika kufikia katika kiwango cha juu cha uongozi wako.
Kufanikiwa kwa kiongozi Zaidi hutokana na wingi wa kujua kwake hivyo ndani ya kitabu hiki ziko hekima nyingi na mafundisho muhimu yenye kukufanya ufikie kwenye ndoto zaka za kiuongozi na kuyadhihirisha mafanikio yako katika uongozi.
Hivyo basi kutokana na umuhimu wa kitabu hiki nanapenda kukukaribisha kufuatilia kwa utulivu na umakini kila kurasa nawe utafurahia na kuona ukibadilika kifikra, kimtazamo, na kiutendaji na kujikuta umekuwa kiongozi aliye fanikiwa
Others Also Bought