Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Books
  • Publish
  • Sell
  • Courses
  • Blog
  • Support

Tabia 5 zinazoleta mafanikio kwa muandishi

February 17, 2021 at 6:51 pm,


Kila muandishi wa vitabu hutaka kufanikiwa lakini mafanikio huchagizwa na tabia anazokuwa nazo muandishi mwenyewe. Kuna tabia tano ambazo muandishi akiwa nazo basi mafanikio huja yenyewe.


1. Andika kila siku. Kuandika kila siku si jambo dogo na pengine wajiuliza, “hili linawezekanaje?”. Lakini unaweza kutenga dakika 5 mpaka 10 kila siku ukaandika, hata kama ni kitu kidogo kiandike. Unaweza kuwa na dakika hizo asubuhi, usiku au mchana wakati. Misuli yako kama muandishi hupashwa kila siku unapoandika.

2. Soma kadri unavyoweza. Huwa wanasema muandishi mzuri ni msomaji mzuri. Soma vitabu vya waandishi mbalimbali, hata vile ambavyo sivyo vya aina unayooandika wewe. Unapofanya hivyo unapata ladha mbalimbali za waandishi wengine na itakufanya kuwa bora zaidi

3. Jiwekee malengo yaliyo wazi. Utapimaje mafanikio yako kama huwezi malengo? Weka malengo yaliyo wazi, yanayopimika.Unaweza kutimiza malengo unayojua, na ambayo unaweza kujikumbusha.

Soma pia: Ufanye Nini Uzinduzi Wa Kitabu Chako Unapofeli?

4. Penda kutumia teknolojia. Muandishi lazimia ujenge tabia ya kwenda na teknolojia. Si muda wote utatumia Microsoft Word kuandika, nenda playstore au appstore na weka evernote. Huwezi kutembela na kalenda kila mahali ili kujikumbusha malengo yako, jizoeze kutumia google kalenda. Zipo teknolojia nyingi mno, jizoeze kuzitumia.

5. Maliza kila unachoanza. Uwe na tabia ya kumalizia vitabu unavyoandika. Najua ni ngumu hii, lakini inawezekana. Kumbuka nguvu uliyoweka ulipoanza kuandika, ukiishia njiani umepoteza muda na nguvu yote uliyoweka. 

Tembelea HAPA kusoma kozi za uandishi wa vitabu bila gharama yoyote



Recent Posts

  • Vitabu Nane (8) vya Elimu ya Fedha - PDF Download
    21 Dec, 2025
  • Tumia mbinu hizi rahisi na uwe miongoni mwa 1% wanaomaliza kusoma vitabu
    5 Dec, 2025
  • Faida za Kuhariri Kitabu kwa Waandishi na Njia za Kukamilisha Uhariri
    1 Dec, 2025
  • Ukitumia njia hizi, utapenda kusoma vitabu
    27 Nov, 2025
  • Siri 5 Unazopaswa Kujua Kutoka Kitabu: Jilipe Mwenyewe Kwanza
    10 Jul, 2025
  • Mambo 10 ya Kujifunza Kutoka Kitabu cha Hamasika Kila Siku
    29 Jun, 2025
  • Download Vitabu 7 vya Fedha (PDF)
    19 Jun, 2025

selling_book-1.png

Enroll in 100% free courses

100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

Start learning →

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Books
  • About us
  • Publish
  • Sell
  • Blog
  • Support
DL Bookstore © 2025. All rights reserved.