Vitabu vitano (5) vya biashara na uchumi muhimu kuvisoma
Mambo yamebadilika sana miaka ya hivi karibuni. Zamani kidogo, watu walikutana na changamoto ya kukosa maarifa muhimu kuhusu biashara na uchumi hasa walipotaka kuanza kufanya biashara au kutaka kujiongezea kipato zaidi. Lakini sasa, vitabu vya biashara na uchumi vimejaa tele kwa wewe kusoma na kufaidika na maarifa ya kukusaidia kufanya biashara bila ugumu wowote.
Tumekuandalia orodha ya vitabu vitano (5) vya biashara na uchumi
ambavyo ni muhimu kuvisoma na vitakuwa kama point of reference
katika biashara na mambo ya uchumi.
1. Tumia Fursa Tengeneza Biashara. Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi Daudi Lubeleje. Mwandishi wa kitabu hiki, kuhusu kitabu chake, anaandika, “Unataka kujifunza jinsi ya kuanza biashara? Unaweza kubadilisha fursa zinazokuja kwako na kuwa biashara. Kitabu hiki ni mahsusi kukupa maarifa ya kutumia fursa na kutengeneza biashara.”. Kinapatikana kwa Tsh. 3999 katika mfumo wa softcopy. BONYEZA HAPA kununua.
2. Deni La Dhahabu. Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi Gastor Mtweve. Mwandishi wa kitabu, kuhusu kitabu chake, anaandika, “Kitabu, “Deni la Dhahabu” ni kati ya vitabu vichache sana sokoni ambavyo vinaweza kubadilisha namna unavyofikiri kuhusu mali na hali yako halisi ya kiuchumi. Chanzo cha umaskini au utajiri ni jinsi mtu awazavyo, “Awazavyo/aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo” (Mithali 23:7). Kama ukiweza kuwaza sahihi kuhusu jambo fulani, utalipata jambo hilo; Na, ukiwaza vibaya kwa namna hasi, bila shaka utalikosa. Mawazo ni vitu, tena vitu halisi; Kitabu hiki kinakupa sio tu namna ya kufikiri lakini pia jinsi ya kufikiri”. Kinapatikana kwa Tsh. 20000 kwa mfumo wa softcopy. BONYEZA HAPA kununua.
3. Mfuko Wa Dharura. Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi Gastor Mtweve. Mwandishi wa kitabu, kuhusu kitabu chake, anaandika, “Jifunze kuhusu fedha, kuweka bajeti, fedhaza majanga na dharura. Kitabu hiki ni msaidizi wako wa kufahamu mambo ya fedha”. Kinapatikana kwa Tsh. 20000 kwa mfumo wa softcopy. BONYEZA HAPA kununua.
4. Jikomboe Kiuchumi Na Ujasiriamali. Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi Linus Siwiti. Mwandishi wa kitabu hiki, kuhusu kitabu chake, anaandika, “Kitabu kizuri kwa anayetaka kuingia katika ujasiriamali. Utajifunza jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile sabuni, mishumaa na n.k”. Kipanatikana kwa Tsh. 6500 kwa mfumo wa softcopy. BONYEZA HAPA kununua.
5. Breakthrough (Mpenyo – VOL 1 & 2). Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi James Mwang’amba. Kuna matoleo mawili; toleo ya kiingereza ambalo linapatikana kwa Tsh. 30000 katika hardcopy, na toleo la kiswahili – 1 & 2 linapatikana katika Tsh. 10000. Kuhusu kitabu hiki, mwandishi anaandika “Ni kitabu kinachokupa nafasi ya kujifunza wapi pakuanzia kama mjasiriamali,mfanyakazi au biashara ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. Wote tunahitaji mtazamo sahihi ili kufanikiwa na kitabu hiki kitakujenga na kukusaidia kufika huko”. BONYEZA HAPA kununua
Kwa vitabu vingi zaidi vya kiroho, hamasa na kadhalika, tembelea duka letu la mtandaoni hapa. Karibu kwa maoni kwenye sehemu ya comments hapa chini.