Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support

Muda na wazazi – Kitabu kipya kutoka kwa Dr. Stanlaus

September 8, 2022 at 4:32 pm,


Ingizo jipya la kitabu kwenye shelfu za vitabu ni kitabu cha MUDA NA WAZAZI ambacho kimeandikwa na Dr. Stanlaus. Kitabu hiki ni moja ya projekti kubwa ambayo tumefanya kuanzia mwezi wa nane na tumeikamilisha mwezi huu wa tisa, tukihusika na kuhariri wake, kusanifu jalada na mpangilio wa ndani wa kitabu. Ni kazi bora sana ambayo tumeifanya.


Mwandishi wa kitabu ametuandikia kionjo kifupi kukuonjesha na kukupa hamasa wewe kukiongeza kitabu hiki katika orodha yako ya vitabu vya kusoma mwezi huu wa tisa. Je, anasemaje mwandishi?

Wazazi ni dhahabu. Wazazi ni thamani kuu kutoka kwa Mungu. Hawa ndio walimu na madaktari wa kwanza wa afya na misingi ya maisha yako. Watu wengi wamekuwa wakianza kuwasahau na kuwapuuzia hasa pale wanapokuwa na kazi, vyeo, biashara kubwa, kiwango kikubwa cha elimu au hata umaarufu. Wameanza kujisahau na kupoteza mafundisho ya msingi yaliyowafikisha pale walipo. Wengine wamewapa majina kama “mizigo, nuksi, au kupitwa na wakati”.

Hali hii imekuwa ikileta mitafaruku na kupoteza amani na furaha baina ya watu hawa wawili yaani mzazi na kijana wake.

  • Je, unataka kufahamu jinsi ya kutambua nafasi ya kila mmoja katika familia?

  • Je, unamfahamu mama au baba ni nani?

  • Je, nafasi yako kama kijana unaitambua vizuri?

Muda na Wazazi ni kitabu mahususi kabisa kwa ajili yako mzazi au kijana wa kileo unayepambana na majukumu yako kwa njia mbalimbali. Kitabu hiki kipo kukupa mbinu, mafunzo na jinsi ya kutoka hatua moja kwenda nyingine bila kumsahau mzazi wako. Usikose nakala yako.

Weka oda ya awali sasa kabla ya uzinduzi rasmi wa kitabu hiki.

Karibu kwa maoni



Recent Posts

  • Umechoka na Minyama Uzembe? Suluhisho la Kupungua Uzito Limepatikana!
    17 Apr, 2025
  • Vitabu Bora vya Pasaka vya Kukuimarisha Kiroho – Vinapatikana Sasa DL Bookstore
    11 Apr, 2025
  • 4 Benefits of Selling Your Book Through DL Bookstore
    20 Mar, 2025
  • Download Entrepreneurship Books (PDF) in Swahili
    10 Feb, 2025
  • Download Nine (9) Must-Read Books for Girls and Women 📚✨
    4 Feb, 2025
  • A Tanzanian Platform for Selling Books Online
    4 Feb, 2025
  • Jinsi ya Kuandika Caption Inayochochea Mauzo ya Kitabu Chako
    23 Nov, 2024

selling_book-1.png

Enroll in 100% free courses

100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

Start learning →

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2025. All rights reserved.