Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Books
  • Publish
  • Sell
  • Learn
  • Blog
  • Support
  • Sign in

Recent Posts

  • Download vitabu 21 vya mahusiano na ndoa
    25 Sep, 2026
  • Book review: ZAKA: Hukumu, Faida na Hekima Zake
    22 Sep, 2026
  • Mfahamu Mwandishi: Khalifa L. Simion - Mwandishi anayeigusa jamii ya Kiislamu
    10 Sep, 2026
  • Mfahamu Mwandishi: Daudi Lubeleje - Mwandishi nyuma ya vitabu 14
    5 Sep, 2026
  • Vitabu 25+ vya Biashara, Fedha na Uchumi
    27 Aug, 2026
  • Book review: Amazing Animal Coloring Book for Kids
    11 Jul, 2026
  • Mapitio ya kitabu: Utambulisho Wako Katika Kristo
    21 Jun, 2026

Categories

  • Book Recommendations
  • Book Reviews
  • Help & Support
  • Offers and discounts
  • Reading Habits & Tips
  • Writing, Publishing & Author Support
  • Author Spotlight

Start selling your book or course on our website — reach more readers

You will enjoy high book visibility, get paid on time and receive a monthly sales report straight to your inbox.

Start selling →

[Kozi] Hatua nne katika uandishi wa vitabu

October 10, 2022 at 11:58 am,


Unazifahamu hatua nne (4) katika uandishi wa vitabu?. Watu wengi hufikia hatua ya kwanza, wengine hatua ya pili na ya tatu, na wachache sana huifikia hatua ya nne. Kuhusu hatua hizi nne (4), fahamu kwamba hatua zote nne zina uzito sawa, halafu zinategemeana, na zinaenda kwa mtiririko kwa kupandiana. Mwandishi hawezi kwenda hatua ya pili, bila ya kupitia hatua ya kwanza.


Je! Hatua hizo nne ni zipi? Tuanze kumla tembo wetu sasa.

Hatua ya kwanza ni KUANDIKA.

Ukitaka kuwa mwandishi wa vitabu sharti uandike kwanza. Iwe wewe mwenyewe utaandika, au utaandikiwa na mwingine, lakini lazima stori yako au maudhui yako yaandikwe.

Hii ndiyo hatua ya kwanza. Karatasi tupu haiwezi kuwa kitabu!. Safari ya kuwa mwandishi inaanza na kuandika. Kaa chini na andika story yako unayotaka iende kwa wasomaji. Kaa chini na andika yale maudhui unataka yafike kwa wasomaji.

Watu wengi hufanikiwa katika hatua hii. Lakini kwa bahati mbaya, vile vitu vingi ambavyo watu wanaandika (bila shaka hata wewe umeandika tayari) wanashindwa kutembea navyo kwenda hatua ya pili katika uandishi ili kukamilisha ndoto zao. Kuishia katika hatua hii ya kwanza hakukufanyi kuwa mwandishi. Kama umeshaandika tayari, fanya juhudi usibakie katika hatua hii ya kwanza ya kuandika tu, bali nenda hatua ya pili.

Kama bado hujaandika, unaanzaje? Nafikiri hili linaweza kuwa swali la wengi. Naanzaje kuandika? Unaanza kuandika kwa kuamua kuandika!. Anza kuandika story yako Facebook, Twitter, WhatsApp au Instagram. Kama unaweza kupiga story kwa masaa matatu na kuzungumza maneno yote hayo huwezi kushindwa kuhamisha hayo maneno kwenye karatasi.

Fanya blogging. Andika machapisho yako na yaweke mtandaoni kwenye blogu. Safari ya uandishi ndivyo inavyoanza hivyo. Hakuna muujiza mwingine wa kuwa mwandishi isipokuwa kuandika kwanza. Kumbuka tu, hii ni hatua ya kwanza itakayokupeleka hatua ya pili. Je! Hatua ya pili ni ipi?

Ili kuendelea kusoma hatua tatu zilizobakia, soma kozi hii katika majukwaa yafuatayo, chagua jukwaa unalopenda

DL Bookstore

DaudiPages

Nyayo zangu

Kwa maswali na maoni, tuandikie hapa chini



Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Books
  • About us
  • Publish
  • Sell
  • Blog
  • Support
  • Sign in
DL Bookstore © 2026. All rights reserved | Made with ❤️ in Tanzania.