Soma vitabu hivi vitatu kama unataka kuwa mwandishi wa vitabu
Nazungumza na mtu anayetaka kuwa mwandishi wa vitabu, kuna vitabu vitatu vya lazima kuvisoma ili upate maarifa ya kukusaidia unapoingia kwenye uandishi wa vitabu.
Vitabu hivi vitakusaidia kupata maarifa muhimu kuanzia hatua ya kuandika, kuandaa, kupiga chapa na kuuza kiabu ulichoandika. Ni vitabu gani hivyo?
1. NAANDIKAJE KITABU?. Kitabu hiki ni toleo lililoboreshwa la kitabu cha Mbinu Rahisi Za Kuandika Kitabu. Wakati nilipotoa kitabu cha Mbinu Rahisi Za Kuandika Kitabu nililenga kuwasaidia watu wanaotaka kuingia kwenye uandishi wa vitabu lakini hawana watu wa kushika mkono ili kufanikisha ndoto zao. Lengo bado ni lile lile isipokuwa nimeboresha zaidi na kufanya marekebisho fulani fulani baada ya kupokea maoni kutoka kwa wasomaji wengi waliosoma kitabu.
Katika toleo hilo jipya, nimeongeza vitu vingi ambavyo naamini, unapokisoma kitabu hiki utatoka ukiwa na nguvu mpya ya kuandika kitabu chako na hatimaye kutimiza ndoto yako ya kuwa mwandishi wa kitabu. Naandikaje kitabu? Ni swali ambalo nimejibu katika kurasa zinazofuata. Mimi naamini, kuandika kitabu ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza.
2. UANDISHI WA KITABU KINACHOUZIKA. Mwenye ndoto ya kuandika na kutoa kitabu ni wewe si mtu mwingine, mwenye ndoto ya kuuza nakala nyingi ni wewe na si mtu mwingine, na mwenye ndoto ya kuwa mwandishi aliyefanikiwa ni wewe na si mtu mwingine. Kwenye hatua yoyote uliyoko sasa; iwe kuandika, kutoa ama kuuza kitabu chako, kitabu hiki kitakuwa msaada kwako.
Unapoanza kusoma kitabu hiki unakuwa umeanza safari ya siku 25 za kuwa mwandishi aliyefanikiwa bila stress. Utafanikiwa kutimiza ndoto yako ya kuandika, kutoa na kuuza kitabu chako kwa mafanikio.Upo tayari kuanza siku 25 za kuwa mwandishi aliyefanikiwa? Upo tayari kuandika kitabu kitakachofika kwa msomaji wako?.
3. KUTOKA KUANDIKA MPAKA KUUZA KITABU. Kwenye kitabu hiki nimeshughulika na mambo matatu;
- Ufahamu wa mbinu za kukusaidia kuandika, kutoa na kuuza kitabu chako. Uandikaje kitabu? Mchakato wa kutoa kitabu ukoje? Kitabu kinafikaje kwa wasomaji na unakiuzaje?. Unapokisoma kitabu hiki, utapata utajiri wa mbinu za kukusaidia kwenye maeneo yote haya
- Ufahamu wa makosa ya kuepuka. Huwezi kuepuka kosa usilolijua, hivyo nimeanza kwa kukuonesha makosa yenyewe ili uweze kuyaepuka. Kuyaepuka makosa haya itakusaidia kuufurahia uandishi wa vitabu kwa kuyachuma mafanikio yake, na
- Kutatua makosa ambayo waandishi huwa wanakwama kupata utatuzi wake. Makosa haya hujitokeza kuanzia hatua ya kuandika mpaka kuuza kitabu. Kusoma kitabu hiki kutakupa kujua jinsi ya kutatua makosa hayo.
Huishii tu kusoma kitabu. Upo huru kabisa kupata usaidizi kutoka kwangu, unapoendelea kusoma kitabu na ukaona kukwama kwenye jambo fulani, wewe nitumie meseji au nipigie, tutazungumza!. Upo tayari kuanza safari nzito ya kusoma sura sita zilizoshiba?.
Kwa nini uandike kitabu? Zipo sababu nyingi lakini kwa uchache; unaongeza njia nyingine ya kupata Kipato, unaacha alama itakayodumu miaka mingi, kitabu hakina mipaka, kinaweza kufika kule usikoweza kufika hivyo mafundisho yako yatafika kwa watu wengi.
Una maswali? Maoni? Nicheki kwenye baruapepe yangu [email protected] au ni WhatsApp hapa
Credit: Chapisho hili limetolewa kwenye blog ya DaudiPages