Bwana, Tufundishe Kusali
Katika Injili ya Mathayo 11:29, Yesu anatoa wito na mwaliko kwa wafuasi wake akisema, "Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyekekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu".
Maneno haya aliyasema mwanzilishi wa imani yetu, baada ya kutoa mwaliko kwa wote wanaolemewa na kusumbuka na mizigo ya kila aina katika mstari wa 28, sasa anatualika sisi tujifunze kwake. Na moja ya vitu tunavyoweza kujifunza kwake ni kuhusu maombi. Nimepewa ufunuo huu kwa ajili ya kanisa, kwa sababu katika nyakati zetu kuna waalimu wengi na watu wengi ambao wanafundisha sana kuhusu maombi lakini si wote wanaofundisha kwa vitendo.
Bali Yesu, Yeye ni mwalimu anayetufundisha kuomba kwa vitendo na katika kitabu hiki ninaamini yapo mengi utakayojifunza ambayo yamkini ulikuwa huyafahamu kuhusu maombi. Mungu anakupenda sana na ana mpango mzuri sana na maisha yako, hivyo kitabu kina msaada mkubwa katika maisha yako, nacho kimebeba majibu ya maswali yako uliyokuwa ukijiuliza kuhusu maombi.
MUNGU AKUPE WEPESI WA KUSOMA NA KUELEWA YOTE YALIYOMO KATIKA KITABU HIKI.
Others Also Bought