Furahini katika Bwana Siku Zote.
Huu ni ujumbe wa muhimu Kwa kila mtu anayekosa furaha kwenye maisha yake au anayekosa changamko la moyo kulingana na mambo mbalimbali yanayoumiza hapa duniani. Kulingana kwamba kila mtu huhitaji kufurahi, kumeibuka sasa wachekeshaji wengi, maigizo ya kuchekesha.
Wengine furaha yao ni uwepo wa watoto , wazazi, mchumba, mwalimu, mchungaji au timu yake ya mpira ikipata ushindi ndiyo siri ya furaha yake. Làkini ukweli ni kwamba furaha inayotegemea watu, vitu au matukio ya nje ya kila siku haina utoshelevu kwenye maisha. Mungu anatamani wakati wote tuwe na furaha haijalishi matukio au watu wanasemaje.
Kwa sababu furaha ni mojawapo ya tunda la Roho Mtakatifu ambalo kila mwana wa Mungu anapaswa kulidhihirisha haijalishi hali ya maisha au watu wasemavyo. Hivyo, kitabu hiki ni mwito wa kipekee kwa kila mtu kuamua sasa kuanza kuishi maisha yenye furaha wakati wote. Kupitia kitabu hiki utajifunza siri nyingi kuhusu kufurahi katika Bwana siku zote.
Machache kati ya mengi yaliyo ndani ya kitabu hiki ni pamoja na ngazi kuu tatu za maisha yenye furaha, utofauti wa furaha katika Bwana na furaha ya nje, ujenzi wa furaha ya kweli katika Bwana siku zote, ukweli kuhusu maisha ya kufurahi kila siku na faida zake.
AMUA SASA KUISHI MAISHA YENYE FURAHA KILA SIKU.
Recommended for you


