Maisha ya vuguvugu yanavyoathiri maisha ya mtu kiroho
Katika safari yangu ya maisha ya kiroho na utumishi wa Neno la Mungu, nimekutana na changamoto nyingi zinazowakumba waamini wa kila aina, wapya na hata wale waliokomaa katika imani.
Mojawapo ya changamoto kubwa, lakini isiyoonekana kwa macho ya kawaida, ni hali ya vuguvugu la kiroho. Hali hii ni hatari kwa sababu inaonekana kana kwamba kila kitu kiko sawa, lakini ndani moyo umepoa, shauku imepungua, na bidii ya kumtafuta Mungu imetoweka.
Kitabu hiki kimebeba mzigo mkubwa kutoka moyoni mwangu, kikiwa na lengo la kufumbua macho ya waamini kuhusu hatari ya kuishi maisha ya kiroho yaliyopoa, pamoja na kuonyesha jinsi hali hiyo inavyoathiri mahusiano yetu na Mungu, huduma, na hatimaye wokovu wetu.
Kwa upendo na kwa msaada wa Roho Mtakatifu, nimejaribu kueleza chanzo cha hali hii, dalili zake, athari zake, na zaidi ya yote, njia ya kutoka kwa yule anayegundua kuwa ameathirika.
Jipatie nakala yako sasa popote ulipo uweze kujiokoa na hatari hii isiyoonekana kwa macho ya kawaida lakini ni hatari sana kwa maisha yako ya kiroho.
Others Also Bought