Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support
  • All books
  • Offers
  • Swahili books
    • Dini
    • Fasihi
    • Maendeleo binafsi
    • Malezi
    • Ndoa na mahusiano
    • Uchumi na biashara
    • Uongozi na usimamizi
    • Vitabu vya kiada
  • English books
    • Business and finance
    • Literature
    • Parenting and relationships
    • Personal development
    • Religion and spirituality
    • Textbooks
  • Children's books
  • Online courses
  • Free books
  • Get books
  • Swahili books
  • Dini
  • Mjue Yesu

Mjue Yesu

TZS 10,000

Paperback eBook
Add to cart  

Kumjua Yesu Kristo ni kwa muhimu kwa ajili ya kukujenga wewe mwana wa Mungu katika kuwa na mahusiano naye ya karibu zaidi.

Kuna tofauti kati ya kujua, kufahamu na kuelewa. Pia, kumjua Yesu si kujua habari za Yesu, si kufahamu historia ya Yesu, si kuelewa kwa akili maandiko kwenye Biblia yanayomwongelea Yesu.

Kumjua Yesu ni kuungana naye binafsi. Kumpokea Yesu binafsi ndani ya moyo wako. Kupokea nuru ya Yesu na makusudi ya kuja kwake hapa duniani.

Macho ya moyo wako yatiwe nuru, upate kufahamu tumaini la mwito wa Yesu, na utajiri wa utukufu wake aliowarithisha watakatifu, na uweza wake uliozidi sana kuwaelekea wanaomwani, uweza huo umo ndani ya wanaomwamini, ni uweza uliomfufua Yesu toka kwa wafu (Waefeso 1:17-20).

Mungu wa utukufu akupe roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye. Usiishie tu kufahamu habari za Yesu kupitia watu, bali yeye mwenyewe akupe kububujika tokea ndani mwako.

Yesu Kristo ni fumbo. Ili kumjua Yesu Kristo ni lazima yeye mwenyewe akufumbulie fumbo hilo.

Kutokana na ukweli kwamba watu wengi hawamfahamu Yesu Kristo, tena hata miongoni mwa wale wanaomwamini; hata kupelekea kubabaika pale wanapokutana na changamoto za maisha yao ya kila siku nimeona vyema kuandika habari za Yesu Kristo kama vile Neno la Mungu linavyotuelekeza.

Kutomfahamu Yesu si tatizo la watu wa siku za sasa tu. Ni tatizo ambalo lilikuwepo tokea siku nyingi, hata wakati Yesu mwenyewe alipokuwapo hapa duniani.


Recommended for you

Historia ya Mitume wa Yesu na Vifo vyao
Historia ya Mitume wa Yesu na Vifo vyao
TZS 5,000
View options
Kuja kwa Yesu Mara ya Pili
Kuja kwa Yesu Mara ya Pili
TZS 10,000
View options
Ufuasi: Agizo Kuu la Yesu Kristo kwa Kanisa
Ufuasi: Agizo Kuu la Yesu Kristo kwa Kanisa
TZS 7,000
View options
Yesu Akawafundisha, Akisema Heri
Yesu Akawafundisha, Akisema Heri
TZS 12,000
View options

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2025. All rights reserved.