Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Moto wa Uamsho wa Roho Mtakatifu
Uamsho Ni Kazi Isiyo Ya Kawaida Ya Roho Mtakatifu Inayozalisha Matokeo Yasiyo Ya Kawaida Katika Kanisa.
Hitaji kubwa la kanisa na ulimwengu leo ni udhihirisho mkuu wa Roho wa Mungu katika nguvu ya uamsho. “Maana rahisi kabisa ya Uamsho ni kurudisha upya uhai. Uamsho ni kuhuisha kile kilicho kufa au kilicho karibu na kufa”.
Kanisa lina hitaji kuamshwa ili liweze kutimiza utume wake. Kanisa lililo kufa haliwezi kamwe kutimiza Utume Uamusho, ndicho basi ambacho Kanisa na ulimwengu vinahitaji. Tunaishi katika nyakati za ukengeufu mkubwa wa kiroho na kuporomoka wa maadili ya kiroho . Kanisa tunahitaji kuamka, tumelala usingizi. Ni uamsho wa Roho Mtakatifu ndio utakao tuamsha.