Mwanafunzi Mwenye Mafanikio
Katika kitabu hiki cha MWANAFUNZI MWENYE MAFANIKIO kitabu kinacholenga kumwandaa mkristo kujitambua na kuishi maisha yenye tija katika ufalme wa Mungu.
Kitabu hiki kinafundisha nanma kanisa la sasa linavyo paswa kuishi ili kuepusha madhara yanayoweza jitokeza kwa kanisa kama yale yaliyotokea katika kanisa la Ulaya na mabara mengine. kanisa la Ulaya na mashariki ya kati lilijisahau na halikuwa na mbinu sahihi zenye kulifanya kanisa hilo kudumu na kurithisha imani kwa kizazi kijacho, mpaka sasa ukristo barani Ulaya umeshuka mpaka kufikia asilimia ndogo sana kiasi cha kufa.
Msisitizo mkubwa wa kitabu hiki ni kuwataka wakristo kuona umuhimu wa kuwa na kudumu katika uanafunzi, kama silaha ya kulijenga kanisa na kulihifadhi na kuhifadhi viwango vyake.
Ukubwa na uzuri wa kanisa si wingi wa watu wala rasili mali wanazomiliki bali ukubwa na uzuri wa kanisa ni mafanikio ya kuwafanya waamini kuwa wanafunzi.
Uanafunzi ni nidhamu ya msingi sana kwa kanisa la Kristo ambapo kila mwamini anapasa kujua kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kujikita katika nidhamu hii ili kuleta mafanikio makubwa katika ufalme wa Mungu. Naamini wazi kuwa utakapokisoma kitabu hiki kwa umakini kitakupatia chachu ya mabadiliko itakayo kufanya kuwa sehemu ya msababishaji wa mafanikio katika ufalme wa Mungu.
Share this book and earn 10%
The author listed this title in our affiliate program. Join the affiliate program to get your own link and earn 10% of every sale you refer.
Others Also Bought