FUNGUO 12 ZA MAFANIKIO
Ni kitabu kinachofungua macho ya msomaji kuelewa kwamba mafanikio si bahati Bali ni matokeo ya mtazamo, maarifa, nidhamu, maamuzi na uthubutu wa kuchukua hatua.
Kupitia FUNGUO 12 muhimu, Noha Lesilwa anachambua kwa kina namna familia, elimu, ajira, kipato, historia, mazingira, umri, na changamoto mbalimbali zinavyoweza kuwa DARAJA AU KIKWAZO cha mafanikio ya mtu
Kwa mtindo wa kisaikolojia, kifalsafa na kifasihi kitabu hiki kinamfanya msomaji ajitafakari upya, kuvunja minyororo ya hofu, na kuona uwezo mkubwa uliopo ndani yake, kupitia simulizi halisi, mifano ya maisha, tafakuri, na mafundisho yenye nguvu, msomaji atajifunza namna ya kubadilisha changamoto kuwa nguvu ya kusonga mbele.
Hiki si kitabu cha hamasa ya muda mfupi pekee, bali ni mwongozo wa kumsaidia mtu kuamsha fikira zake, kujenga maisha makubwa, na kuanza safari ya mafanikio yenye maana ya kweli.
Kama umewahi kuhisi kama umechelewa, umekwama, au mazingira yako hayawezi kukuruhusu kufanikiwa - Basi kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili yako
Others Also Bought