Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Hujachelewa kufanikiwa
Siyo kwamba kitabu hiki kinakupa ruhusa ya kuendelea kuchelewa kutekeleza jambo fulani katika maisha yako. Bali nguvu ya neno ‘HUJACHELEWA KUFANIKIWA’ katika kitabu hiki ni kuonesha bado kuna jambo unaweza kulifanikisha hasa pale ulipoona haiwezekani au umechelewa sana. Hivyo kwa kutumia mifano halisi, utafiti juu ya mambo mbali mbali yanayowachelewesha watu wengi kuanza safari ya ndoto zao, kanuni zilizotumika na njia mbadala zilizowafanya watu wengine kufanikisha mambo mbali mbali na makubwa.
Ni imani yangu uchambuzi na uandishi wa kitabu hiki utakupa sababu zenye nguvu ya kuanza safari ya utatuzi wa yale unayoyaona kama vikwazo katika maisha yako. Sababu zenye nguvu ya kwanini ufanikiwe badala ya kutokufanikiwa. Mwisho, kitabu hiki kinatoa fursa ya MKATABA WA MALENGO ambao ni msingi wa mafanikio, kinyume na mikataba mingi ambayo ni matokeo ya malengo yasiyothaminiwa.