Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Nguvu ya Pasaka katika Kushinda Vita ya Kiroho
Vita ya kiroho ni mapambano katika ulimwengu wa roho kati ya UFALME WA NURU dhidi ya UFALME WA GIZA na vita hii ni halisi kabisa lakini kwa kukosa ufahamu na uelewa wa vita hii. Shetani na washirika wake wametumia nafasi hii kuwashambulia watu wengi kwa njia mbali mbali, pamoja na mashambulizi hayo Mungu amewapa watu wake mamlaka na uwezo mkubwa wa kutumia NGUVU YA SILAHA YA PASAKA kwa ajili ya KUJILINDA na KUMSHAMBULIA shetani.
Lakini tatizo kubwa lililopo kwa watu wengi ni kukosa ule ufahamu wa vita yenyewe ya kiroho, utambuzi wa nguvu ya silaha ya Pasaka na namna ya kuitumia kwa ufanisi katika kumshinda shetani. Hivyo nimeandika kitabu hiki ili kikusaidie na kukujengea uwezo wa kufahamu,kuelewa na kujitegemea katika mapambano dhidi ya shetani kwa kutumia nguvu iliyomo katika silaha ya Pasaka.
Naimani kwa njia ya kitabu hiki utaweza kujifunza mbinu mbali mbali unazoweza kuzitumia kumtambua adui, utambuzi wa silaha mbali mbali katika kushinda vita ya kiroho, jinsi ya kutumia silaha ya nguvu ya Pasaka katika maombi na uhakika wa kushinda katika vita ya kiroho.