Saikolojia na Maisha ya Kikristo
Mungu alimuumba mwanadamu kwa njia tofauti na kiumbe kingine chochote, yaani kwa mfano na sura yake isiyoonekana katika mwili. Lakini baada ya anguko, dhambi iliharibu asili ya mwanadamu na kusababisha kufanya dhambi kuwa jambo lisiloepukika. Mungu alitoa sheria katika mlima Sinai lakini sheria haijamsaidia mwanadamu kufikia viwango vya utakatifu wa Mungu.
Kwa upande mwingine Saikolojia inajaribu kuainisha tabia za mwanadamu zinazotokana na asili yake iliyoharibiwa na dhambi ili kumsaidia kubadili tabia yake na kuushinda udhaifu alionao na kuboresha mahusiano yake na wengine. Hata hivyo mwanadamu amejaribu kubadili hali hiyo kwa juhudi zake mwenyewe mbali na Mungu bila mafanikio. Kwa mfano, uzoefu unaonyesha kuwa pamoja na ushauri wa kisaikolojia, bado watu wengi wameendelea kuishi sawa sawa na haiba zao.
Ukristo unakuja na suluhisho kwa kuonyesha kuwa mwanadamu akimwamini Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake atazaliwa mara ya pili na kuwa kiumbe kipya. Ikiwa watu watapokea kweli ya Neno la Mungu, hawahitaji msaada mwingine wowote. Lakini kama mtu ataikataa Injili, basi katika hali fulani, saikolojia ni bora kuliko kile alicho nacho. Pia baadhi ya watu, kwa sababu mbalimbali, wanahitaji msaada zaidi maalumu wa kisaikolojia katika kushughulika na kushinda vikwazo vya kuishi maisha ya kumcha Mungu.
Join our WhatsApp Channel
Get book offers and discounts, new release updates, book reviews, recommendations and more. Follow the channel →
Share this book and earn 10%
The author listed this title in our affiliate program. Join the affiliate program to get your own link and earn 10% of every sale you refer.
