Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Books
  • Publish
  • Sell
  • Courses
  • Blog
  • Support
  • All books
  • Discounts
  • Swahili books
    • Afya na ustawi
    • Dini
    • Fasihi
    • Malezi
    • Ndoa na mahusiano
    • Maendeleo binafsi
    • Uchumi na biashara
    • Uongozi na usimamizi
    • Vitabu vya kiada
  • English books
    • Business and finance
    • Health and wellness
    • Literature
    • Parenting and relationships
    • Personal development
    • Religion and spirituality
    • Textbooks
  • Children's books
  • Online courses
  • Free books
  • Books
  • Swahili books
  • Dini
  • Sauti ya Imani

Sauti ya Imani

  10,000.00 TZS

eBook
Add to cart  

2 Timotheo 4:3-4 “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima, ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti, nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo” (KJV)

2 Timotheo 4:3-4 “Maana wakati utakuja watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye uzima. Badala yake, ili kutimiza tamaa zao wenyewe, watajikusanyia idadi kubwa ya walimu wapate kuwaambia yale ambayo masikio yao yanayowasha yanatamani kusikia. Watakataa kusikiliza kweli na kuzigeukia hadithi za uongo.” (NIV)

Kile kizazi ambacho mtume Paulo alikisema, sasa kimeshawadia, ndio hiki tulichonacho sasa. Kizazi ambacho hakitaki kabisa kusikia mafundisho ambayo yana uzima ndani yake bali wanachagua kusikia mafundisho wanayoyataka wao ambayo hayana uzima bali yanawaburudisha tu.

Kutokana na kuwa na sauti nyingi za kigeni katika nyakati hizi za mwisho imewafanya wakristo wengi kupoteza imani zao za kweli kwa kuzitoa kwa  Mungu  wao  anayeweza  kuwaokoa  na

kuzipeleka kwa vitu visivyoweza kuokoa.

Kwa kuwa chanzo cha Imani ni Neno la Mungu, kuna watu wengi wamejiingiza kufundisha neno kwa jina la wahubiri lakini hawahubiri neno la Kristo bali mambo ya kuhamasisha tu watu kujipambania maisha yao, na hivyo imepelekea wakristo wengi kuzigeukia sauti hizo ambazo zimeua kabisa imani hiyo.

Na hata wale wanaosikia neno la kweli bado wanashindwa kuamini na hata wale wanaoamini nao wanashindwa kufanya matendo ya imani na hivyo wengi kushindwa kuyaona matokeo ya imani yao.

Kitabu hiki ni kwa ajili ya kuhuisha shauku iliyopotea ya kusikia Neno la Mungu lenye uzima na kuzaa tena imani ndani yako.


Others Also Bought

IMANI ILIYO HAI KATIKA ULIMWENGU WENYE KELELE
IMANI ILIYO HAI KATIKA ULIMWENGU WENYE KELELE
5,000.00 TZS 3,000.00 TZS
Safari ya Imani
Safari ya Imani
4,000.00 TZS
HILI NI NENO LA KUFAA KWAKO - Siku 21 za kukua, kujijenga na kujiimarisha kiroho
HILI NI NENO LA KUFAA KWAKO - Siku 21 za kukua, kujijenga na kujiimarisha kiroho
9,999.00 TZS 7,500.00 TZS

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Books
  • About us
  • Publish
  • Sell
  • Blog
  • Support
DL Bookstore © 2026. All rights reserved | Made with ❤️ in Tanzania.