Ujue Ulimwengu wa Ndoto Kibiblia
Ulimwengu wa roho ni ule ulimwengu usioonekana kwa macho ya kawaida. Kama kuna ulimwengu wa roho maana yake kuna ulimwengu wa mwili. Ulimwengu wa mwili ni huu ulimwengu wa kawaida tunaouona na vitu vilivyomo. Ni rahisi kuuelewa ulimwengu wa mwili lakini si rahisi kuuelewa ulimwengu wa roho. Ulimwengu wa ndoto ni sehemu ya ulimwengu wa roho. Mafunuo sahihi kuhusu ndoto yanahitaji ushirika wa Roho Mtakatifu kwa sehemu kubwa. Kwanini Roho Mtakatifu? Soma 1 Wakorintho 2:10-16.
Mungu anatufunulia sote siri za rohoni kupitia Roho Mtakatifu. Ukimkwepa Roho Mtakatifu ujue umekwepa sir za rohoni ikiwemo maarifa kuhusu ulimwengu wa ndoto. Roho Mtakatifu ndiye afisa uchunguzi wa mambo yote yanayoendelea rohoni. Ukipata shida ya vitu vya rohoni mwalike Roho Mtakatifu akusaidie kuchunguza na kupata ufumbuzi. Rohoni kuna mafumbo ya Mungu ambayo mwenye majibu ni
Roho Mtakatifu peke yake. Hakuna njia fupi ya kuyajua mafumbo ya Mungu bila kumhusisha Roho Wake. Roho Mtakatifu ni zawadi kwa kila aliyeokoka ili amsaidie kila mmoja kujua aliyokirimiwa au aliyowekewa amana na Mungu. Uwezo wa kuyanena na kuyakiri tuliyokirimiwa bado unadai lugha ya Roho Mtakatifu. Ukiona unakiri ushindi hata wakati huuoni na unaamini wewe ni mshindi ujue huyo sio wewe bali Roho Mtakatifu ambaye tayari anaziona zawadi zako zote zilizopo rohoni. Kwa hiyo acha kujidharau. Roho Mtakatifu anafanya kazi na watu wa tabia ya za rohoni tu.
Mengi yaliyoandikwa kwenye kitabu hiki kuhusu ulimwengu wa ndoto yanatambulikana kwa msaada wa Roho Mtakatifu na kwa sehemu kubwa kimebeba mifano hai kuliko nadharia. Karibu ujifunze.
Others Also Bought