Vita ya Madhabahu Dhidi ya Hatima Yako
Katika kitabu hiki cha VITA YA MADHABUHU DHIDI YA HATIMA YAKO, ni ujumbe wa mafunuo ambayo Mungu ameachilia ndani yangu kwa lengo la kuwasaidia watu mbalimbali ili waweze kuishi kwa mafanikio katika maisha yao yote wawapo hapa duniani wakati wakiongozwa na madhabahu zao.
Maisha yote ya mwanadamu ili afanikiwe inategemea sana namna vile anavyohusiana na madhabahu yake. Kazi kubwa ya madhabahu juu ya mwanadamu ni kumuunganisha mwanadamu na Mungu wake; kwani mwanadamu utoshelevu wa maisha yake hutegemea sana mahusiano yake na Mungu wake.
Watu wengi wamekosa taarifa na maarifa sahihi ya namna ya kuishi katika madhabahu zao, hivyo hupelekea kuishi pasipo kujali taratibu za kimadhabahu kitu kinacho sababisha kuishia kwenye matatizo na maisha magumu kutokana na kukiuka maadili, miiko, sheria, Desturi na maagano ya madhabahu.
Mateso ya wengi katika madhabahu si tu kwa sababu ya hasira ya shetani juu ya maisha yao, ila ni kutokana na kutojua namna ya kuishi katika madhabahu zao.
Mara zote makosa husababisha gharama kubwa katika maisha ya watu, ijapokuwa wameyafanya kwa sababu ya kutojua na kukosa maarifa au Elimu. Kumbuka ukikosea gharama ya makosa yako haiondolewi au haipungui kwa sababu wewe hukujua bali utalazimika kulipa gharama tu.
Kitabu hiki kinafundisha namna madhabahu inavyohusika na kufanya kazi katika maisha ya watu na namna sahihi ya kuishi kwenye madhabahu kutakako kuletea mafanikio katika maisha yako yote ya hapa duniani.
Kitabu hiki sio tu kinakufundisha namna ya kuishi maisha ya mafanikio katika madhabahu yako, bali kinakufundisha namna ya kuwa na mahusiano bora na yenye mafanikio kwa Mungu wako
Others Also Bought