Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Chochea Kipaji Chako
Kitabu hiki ni nyenzo muhimu kwa mtu mwenye kipaji. Zipo kanuni na mbinu muhimu za kumsaidia kila mwenye kipaji kufanya vizuri sokoni. Pesa hufuata harufu ya ubora. Ukifanya kwa ubora kwenye kipaji chako lazima watu wanaofaidi kipaji chako wakulipe vizuri. Tatizo ni kwamba ubora hauji kimiujiza, bali ni matokeo ya kutumia kanuni sahihi na mbinu zilizo bora. Basi, kitabu hiki ni lazima kwako kukisoma ili ufaidike na maarifa yaliyo ndani yake.
Mara nyingi wanaobaki kwenye ushindani na kuendelea kufanya vizuri ni wale wanaopata mbinu mpya katika maeneo ya vipaji vyao. Ndani ya kitabu hiki zimeelezwa njia za 4 kugundua kipaji chako na haijaishia hapo, Pia kuna mbinu za kuchochea kipaji chako baada ya kukigundua. Mbinu 5 muhimu zilizoelezwa ni;
- Badili chanzo chako cha taarifa
- Badili watu unaombatana nao
- Ongeza maarifa/ujuzi
- Jiandae nyuma ya pazia
- Maombi
Usiache kutumia kipaji chako. Usiache kuchochea kipaji chako. Jambo la muhimu zaidi, kipaji chako kisikutoe kwa Mungu. Unaposoma kitabu hiki utagundua kwamba, mwandishi anaweka mkazo, kuchochea kipaji chako huku uhusiano wako na Mungu ukiimarika zaidi.