Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
One More Plague: Pigo Moja la Mwisho
ONE MORE PLAGUE.
Tunahitaji faraja kuliko huzuni, tunahitaji amani kuliko vita, tunahitaji mafanikio na siyo umasikini lakini kufikia kwenye hatua hii inawezekana.
Mtu mmoja aliwahi kusema "if you think you can or you cannot, in either way you are probably right" uwezo wa Kila kitu kufanyika hutegemea maamuzi ya busara kutoka Kwa mhusika. Pengine unakitu ndani yako na unatamani kufikia malengo lakini unashindwa namna ya kuanza, basi kitabu hiki kitaenda kukufaa zaidi.
Pengine umejaribu mbinu nyingi kutimiza ndoto zako lakini umekwama na ukakata tamaa, pengine ndiyo umeanza lakini bado unaona Kuna ugumu. Kitabu hiki kitaenda kufungua mambo mengi yaliyofungwa katika safari ya mafanikio yako.
Ndani yako Kuna nguvu kubwa, wewe ni shujaa, Mungu amekupa kutawala na kumiliki. Mwamshe shujaa ndani yako. Acha mwanga ulio ndani yako ung'ae na uangaze .
Nakukaribisha Sasa kusoma kitabu hiki na Mungu akutangulie na kukupa ufahamu wa kuelewa maarifa ya kukupeleka mahali pazuri ndani ya kitabu hiki.