Siri za mwanafunzi bora
Mpendwa Msomaji,
Karibu katika kitabu Siri za Mwanafunzi Bora.
Ninakushukuru kwa kuchukua muda wako kukisoma. Huenda wewe ni mwanafunzi, mzazi, au mwalimu, lakini ninaamini umefika hapa kwa sababu muhimu.
Kwa miaka kadhaa nikiwa mwalimu, nimeona wanafunzi wengi: wenye uwezo mkubwa lakini wasio na nidhamu, waliokata tamaa baada ya kufeli, na waliopotea kwa sababu ya marafiki wabaya au matumizi mabaya ya teknolojia. Pia nimeona wanafunzi waliobadilika kabisa walipopata mwongozo sahihi.
Uzoefu huo ulinifundisha kuwa:
Mwanafunzi bora hazaliwi akiwa bora; hujengwa kwa maamuzi sahihi, nidhamu, juhudi, mwongozo mzuri na hamu ya kujifunza kila siku.Ndiyo sababu niliandika kitabu hiki.
Lengo langu ni kukupa mwongozo wa vitendo utakao kusaidia kujitambua, kujenga tabia nzuri za kujifunza, kushinda uvivu, kutumia teknolojia kwa manufaa, kujiamini na kuendelea kupambana na changamoto.
Katika kurasa hizi utajifunza siri muhimu za mafanikio ya mwanafunzi, pamoja na nafasi ya wazazi na walimu katika kumlea mwanafunzi mwenye maadili, nidhamu na ndoto kubwa.
Nakuomba usome kitabu hiki kwa utulivu, tafakari kila ujumbe na uanze kuutumia katika maisha yako. Maarifa yana thamani yanapowekwa katika vitendo.
Others Also Bought