Maswali 5 ya kujiuliza kama jalada la kitabu linafaa

Jalada la kitabu linaweza kuwa ni zana yako muhimu katika mauzo ya kitabu chako au likawa ni ukuta wa wewe kutouza vitabu vyako. Bidhaa yoyote huwa na kifungashio chake cha kumvuta mteja anunue, na wewe kama muandishi, kifungashio chako ni jalada la kitabu. Ili kuruka kiunzi cha kupata jalada lisilouza, jiulize maswali haya 5 kabla ya kuamua jalada ulilonalo litumike kwenye kitabu;
1. Je jalada la kitabu linaendana na toni na aina (tanzu)
ya kitabu chako?. Jalada zuri la kitabu lafaa libebe toni na aina ya kitabu
ulichoandika. Mfano, kama ni kitabu cha riwaya kinachozungumzia mapenzi, basi jalada
lake lizungumze mapenzi pia ili msomaji avutike kusoma yaliyo ndani ya kitabu.
2. Je jalada la kitabu linatofautisha kitabu chako na
vitabu vya waandishi wengine katika tanzu inayofanana?. Jalada la kitabu chako
lisifanane kabisa na jalada la kitabu cha muandishi mwingine ambaye mmeandika,
mfano riwaya za mapenzi. Lazima kuwe na tofauti.
3. Je jina la kitabu linasomeka vizuri hata kama
picha ya jalada ikipunguzwa ukubwa wake?. Inapotokea picha ya jalada la kitabu
inapugunguzwa ukubwa wake, basi jina la kitabu liendelee kuonekana na kusomeka
vizuri. Mfano, jalada linapotumika kwenye tangazo la kutangaza kitabu chako
mtandaoni.
4. Je unahitaji jalada la kitabu litumike kwenye
nakala ngumu, nakala laini au vyote kwa pamoja?. Sifa ya jalada bora la kitabu
ni uwezo wa kutumika unapotoa nakala ngumu au nakala laini, pasipo kupoteza
ubora wake. Lakini wewe kama muandishi, jalada lako linapotengenezwa, chagua
mapema linatumika wapi?
5. Je jalada la kitabu litafanya kitabu chako
kionekane zaidi ya vingine katika duka la vitabu?. Duka la vitabu halitakuwa na
kitabu chako tu pekee, vitabu vipo vingi mno, na kitabu chako lazima kionekane
kwa haraka kuliko vitabu vingine. Jalada bora lazima lifanye kitabu chako
kionekane zaidi.
Pata ofa ya kitabu cha Mambo 7 Usiyoyajua Kuhusu Dhambi kabla ya tarehe 17/10/2020 kwa Tsh. 3500 badala ya Tsh. 5000, Hardcopy au kwa Tsh. 2500 badala ya Tsh 3999, softcopy sasa.
