Kila mtu mwenye njaa ya mafanikio, hivi ndivyo vitabu vya kusoma.
Ukiiwaza kesho yako itakuwaje, utapata njaa ya mafanikio. Kocha wa mpira wa kikapu, John Wooden aliwahi kusema “Mafanikio ni amani ya akili, ambayo ni matokeo ya moja kwa moja ya kujiridhisha kwa kujua umefanya juhudi za kuwa bora”. Njia mojawapo ya kupata amani ya akili ni kusoma vitabu. Kwa kusoma vitabu unaanza kuona ni wapi uelekeze hustle zako ili upige hatua zaidi.
Badala ya kukata tamaa kwa sababu huishibishi njaa yako ya mafanikio, soma vitabu hivi ambavyo vitakupa boost ambayo umekuwa ukiitafuta kwenye safari yako ya kusaka mafanikio.
1. Usijizuie kufanikiwa. Tofauti na vitabu vingi, kitabu hiki kimegusa maeneo mengi ya muhimu yanayohitajika ili mtu afanikiwe.
Ukweli ni kuwa watu wengi wamekuwa wakihangaika kutafuta mbinu za kufanikiwa kwenye maisha yao, Wanahangaika kutafuta sababu za nje bila kujua wao ndiyo kiini cha kutokufanikiwa kwao.
2. Umezaliwa kufanikiwa. Sayansi ya Mafanikio inathibitisha kuwa kila mtu mwenye uhai duniani ana haki na nyenzo zote za kufanikisha malengo yake makubwa, mahali popote alipo na kwa wakati wowote kama akiamua.
Watu wengi wasiofanikiwa huwa wanafikiri kuwa wao hawana haki yakufanikiwa, ila ukweli ni kuwa hakuna mtu aliyeumbwa ili asifanikiwe na ndio maana kila mtu ana uwezo wa kipekee kabisa ambao ndio nyenzo ya mtu kufikia Mafanikio yake makubwa.
3. Hujachelewa kufanikiwa. Siyo kwamba kitabu hiki kinakupa ruhusa ya kuendelea kuchelewa kutekeleza jambo fulani katika maisha yako. Bali nguvu ya neno ‘HUJACHELEWA KUFANIKIWA’ katika kitabu hiki ni kuonesha bado kuna jambo unaweza kulifanikisha hasa pale ulipoona haiwezekani au umechelewa sana.
Hivyo kwa kutumia mifano halisi, utafiti juu ya mambo mbali mbali yanayowachelewesha watu wengi kuanza safari ya ndoto zao, kanuni zilizotumika na njia mbadala zilizowafanya watu wengine kufanikisha mambo mbali mbali na makubwa.
4. Mwongozo katika mafanikio. Kitabu hiki cha MWONGOZO KATIKA MAFANIKIO ni kitabu ambacho kimelenga sehemu zote kukuongoza kukupa matokeo mazuri ya maana halisi ya mafanikio yako bila kukutenga au kukuondoa nje na mtizamo wako wa mafanikio.
Kitabu hiki kimebeba majibu ya maswali mengi ambayo umekuwa ukijiuliza na kujitia wasiwasi ndio maana tumekiita MWONGOZO KATIKA MAFANIKIO kwasababu kama kweli utakuwa umejitoa katika kufanya yale ambayo utayakuta katika kitabu hiki jua tayari utakuwa umeshaweka msingi wako wa mafanikio na kitakachobaki ni wewe kuendelea na ujenzi wako kwa kujitoa na kuwa na imani kwamba mwisho utafika na utadumu zaidi katika vizazi na vizazi.
Usisahau!, kuna vitabu vingi sana kwenye duka letu la mtandao, tembelea hapa na jichagulie kitabu unachopenda kusoma.
Una maoni yoyote kwetu? Tuandikie kwenye comment hapa chini.