Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Books
  • Publish
  • Sell
  • Courses
  • Blog
  • Support
  • Sign in

Recent Posts

  • Mfahamu Mwandishi: Khalifa L. Simion - Mwandishi anayeigusa jamii ya Kiislamu
    10 Sep, 2026
  • Mfahamu Mwandishi: Daudi Lubeleje - Mwandishi nyuma ya vitabu 14
    5 Sep, 2026
  • Vitabu 25+ vya Biashara, Fedha na Uchumi
    27 Aug, 2026
  • Book review: Amazing Animal Coloring Book for Kids
    11 Jul, 2026
  • Mapitio ya kitabu: Utambulisho Wako Katika Kristo
    21 Jun, 2026
  • Mapitio ya Riwaya: Mimi Ashraf
    3 Jun, 2026
  • Vitabu 6 Bora vya Uwekezaji na Uhuru wa Kifedha kwa Kiswahili
    20 May, 2026

Categories

  • Book Recommendations
  • Book Reviews
  • Help & Support
  • Offers and discounts
  • Reading Habits & Tips
  • Writing, Publishing & Author Support
  • Author Spotlight

Start selling your book or course on our website — reach more readers

You will enjoy high book visibility, get paid on time and receive a monthly sales report straight to your inbox.

Start selling →

Mfahamu Mwandishi: Khalifa L. Simion - Mwandishi anayeigusa jamii ya Kiislamu

September 10, 2026 at 2:35 pm,

Mfahamu Mwandishi: Khalifa L. Simion - Mwandishi anayeigusa jamii ya Kiislamu

Kama nyuki anayezunguka takribani maua 4,000-5,000 ili kutengeneza mililita moja ya asali ambayo mnywaji anaweza kunywa mara moja na kuimaliza, vivyo hivyo waandishi huzunguka vyanzo vingi vya maarifa na tafsiri wakikusanya vipande vidogo vya hekima na kuviunganisha kwa juhudi kubwa, na msomaji hunufaika kwa kitabu kimoja ambacho anaweza kukisoma na kukimaliza mara moja; hivyo, mfano huu unatosha kuwa motisha kwa wenye akili, na unafupisha kwa uwazi faida ya kusoma na kunufaika kutoka kwenye vitabu.

Khalifa Loishorwaki Simion alizaliwa Arusha, Tanzania, na kwa sasa anaishi jijini Dar es Salaam. Ni mhitimu wa shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar, Cairo, Misri (mwaka 2020) – moja ya vyuo vikongwe na vyenye heshima kubwa zaidi duniani katika masomo ya dini ya Kiislamu. Elimu hii imemjengea msingi imara wa kuchambua na kufundisha masuala ya kidini kwa umahiri na uaminifu.

Pata vitabu vyote vya Khalifa hapa

Khalifa alianza safari yake ya uandishi tangu mwaka 2015, akiwa na shauku ya kuunganisha elimu ya dini na maisha halisi ya jamii. Kitabu chake cha kwanza, Methali na Uislamu, kinaunganisha hekima za methali za Kiswahili na mafundisho ya Kiislamu, kikionyesha jinsi busara za jadi zinavyoendana na misingi ya dini. 

Tangu hapo, ameendelea kuandika vitabu vinavyolenga kufafanua masuala ya kiibada na kimaisha kwa uwazi na usahihi – ikiwemo kitabu chake cha hivi karibuni, Zaka Katika Uislamu: Hukumu, Faida na Hekima Zake, kinacho mwongoza msomaji kuelewa na kutekeleza nguzo hii muhimu ya tatu ya Kidini, hata katika masuala ya kisasa kama mishahara, akiba za mtandaoni, na uwekezaji.

"Na Chochote Mtakacho Kifanya Katika Kheri Allah Anakijua." (Āl ‘Imrān: 92)

Vitabu vilivyochapishwa:

  1. Methali na Uislamu (2015)
  2. Mwongozo wa Maisha ya Kila Siku (2024)
  3. Swala kwa Vitendo: Udhu, Kuoga na Tayamum (2026)
  4. 99 za Fiqhi (2025)
  5. Mtume Wangu (s.a.w) (2025)
  6. Safari ya Kumjua Mola Wangu (2025)
  7. Zaka Katika Uislamu (2026)

Tembelea hapa duka la Khalifa ujipatie vitabu hivi vyote kwa pamoja

Khalifa Loishorwaki Simion – Mwandishi | Shams Academy - Kitengo cha Dini

📧 Barua pepe: [email protected] 📞 Namba ya Simu: +255757100491 / +255711753666



Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Books
  • About us
  • Publish
  • Sell
  • Blog
  • Support
  • Sign in
DL Bookstore © 2026. All rights reserved | Made with ❤️ in Tanzania.