MFAHAMU MWANDISHI: DAUDI LUBELEJE - Mwandishi nyuma ya vitabu 14
Unaweza kuandika vitabu 14 kwa sababu tu unapenda kuandika? Kwa Daudi Lubeleje, jibu ni ndiyo.
Daudi alianza safari yake ya uandishi wa vitabu mwaka 2016, na kitabu chake cha kwanza kilikuwa Mambo 7 Usiyoyajua Kuhusu Dhambi. Tangu wakati huo, ameendelea kuandika vitabu mbalimbali vinavyogusa imani, maendeleo binafsi, uandishi, biashara na uwekezaji.
Kitabu chake cha hivi karibuni ni Hisa, Hatifungani,Vipande: Uwekezaji kwa Ukuaji wa Mtaji na Kipato Endelevu, kinachozungumzia uwekezaji na namna ya kujenga mtaji na kipato endelevu.
Vitabu alivyoandika
- Mambo 7 Usiyoyajua Kuhusu Dhambi
- Mduara wa Dhambi
- Chochea Kipaji Chako
- Mambo Muhimu kwa Mwalimu wa Biblia Unapoandaa Somo
- Ushindi katika Hali Ngumu
- Sadaka ya Fungu la Kumi ni Nini?
- Uandishi wa Kitabu Kinachouzika
- Tumia Fursa Tengeneza Biashara
- Kutoka Kuandika Mpaka Kuuza Kitabu
- Naandikaje Kitabu?
- HILI NI NENO LA KUFAA KWAKO – Siku 21 za Kukua, Kujijengana Kujiimarisha Kiroho
- Mbinu Rahisi za Kuandika Kitabu
- Utumishi Unaotimiza Mapenzi ya Mungu
- Hisa, Hatifungani, Vipande: Uwekezaji kwa Ukuaji wa Mtajina Kipato Endelevu
Lakini siri ya Daudi kuandika vitabu vingi si kwamba ana mbinu fulani ya kichawi. Anapenda kuandika.
Anapokaa kuandika, anaweza kutumia masaa mengi bila hata kutambua muda umepita. Kwake, kuandika si jambo analolazimisha kufanya; ni kitu anachofurahia.
Mbali na uandishi wa vitabu, Daudi ni mwanzilishi wa DaudiPages Academy, inayowasaidia watu kujifunza mambo mbalimbali kuhusu uandishi wa vitabu—kuanzia kupata na kuendeleza wazo, kuandika kitabu, hadi kukitoa na kukiuza. Pia hutoa kozi mbalimbali za uandishi pamoja na one-to-one mentorship kwa waandishi.
Na anapokuwa si kwenye uandishi? Anapenda kusoma vitabu vya waandishi wengine na kupiga gitaa.
Huyo ndiye Daudi Lubeleje—mwandishi, mwalimu wa waandishi, msomaji wa vitabu na mtu anayefurahia sana mchakato wa kuandika.
Ungependa kusoma vitabu vyake?
DL Bookstore inakualika kuvipata vitabu vya Daudi Lubeleje.
Kama ungependa kusoma zaidi ya kimoja, chagua vitabu unavyotaka kwenye bundle yako na tutakupatia punguzo kubwa la bei. Tuandikie kwenye comment au bofya hapa kuwasiliana nasi
Je, umewahi kusoma kitabu cha Daudi Lubeleje? Ni kipi?