Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Njia Anazotumia Roho Mtakatifu Kutufikishia Ujumbe Wake
Kitabu hiki kinahusu, njia ambazo Roho Mtakatifu huzitumia mara kwa mara kutufikishia ujumbe wake kuhusiana na kila jambo linalo husu Maisha ya mtu husika. Tukumbuke Neno la Mungu kutoka kitabu cha Amosi 3:7 linasema “Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.”
Niliyo ya andika katika kitabu hiki ni baadhi ya uelewa wangu kuhusu njia, lugha na sauti ya Mungu, kulingana na vile ambavyo Mungu Roho Mtakatifu amekuwa akizitumia kuzungumza nami kwa muda wa miaka niliyodumu katika wokovu. Kwa hiyo usomapo kitabu hiki, utapata maarifa ya sehemu muhimu katika ufalme wa Mungu, yatakayo kufanya uelewe vingi vinavyo husiana na ufalme wake, wewe na kila atakachopenda kukufunulia.
Kitabu hiki kitakusaidia kuamsha ari ya kumkaribia Mungu kwa njia ya sala ya utulivu, kuongeza neema ya karama ambazo Mungu amekuzawadia ulipo batizwa na kumpokea Rogho Mtakatifu. Ikiwa utapata kuelewa jinsi Mungu anaweza kuzungumza nawe, kwa ukaribu huu wa Mungu katika Maisha yako, unakuwa mtu ambaye si rahisi kubebwa na hila za adui (shetani). Hivyo kitabu hiki kitakupa uwezo wa kupambanua kila jambo kwa mtazamo wa Roho na kuliendea kwa usahihi.
Mambo hayo yanahitaji imani iliyo thabiti mbele za Mungu na uelewa mzuri katika yote ambayo Mungu anakuwa anaachilia juu ya mtu husika. Pia inahitajika hekima, busara, na maarifa katika utekelezaji mbele za Mungu na wanadamu.
Sisemi kuwa nimekamilika katika hayo au ninaelewa sana yote nizungumzayo katika kitabu hiki, hapana! Kwakuwa sote kwa mambo ya rohoni, tunafahamu kwa sehemu. 1 Wakorintho 13:9,12. Ni kwa nafasi ndogo tu, ya uelewa ambao Mungu amenipa, niliona si vema kubakiwa nayo peke yangu maarifa hayo, bila kuwashirikisha wengine wa karibu yangu na walio mbali nami wenye uhitaji.
Ni ombi langu mbele za Mungu kuwa atoe kibali cha uelewa wa kimbingu kwa wewe utakaesoma kitabu hiki, ili uweze kuishi karama na vipaji ulivyojaaliwa na Mungu kwa usahihi, katika huduma na maisha kwa ujumla. Kwakua kuzifahamu njia za Mungu, ni mwanzo wa kumjua yeye na kuzipata neema zake. Kutoka 33:13.
Nakupongeza kwakuwa umechagua fungu jema, kujipatia nakala ya kitabu hiki. Mungu mwema akubariki sana.