Mtu wa tofauti
Watu wa kawaida ni wengi sana ndio maana ni rahisi kuwatambua watu wa Tofauti. Huwezi kuwa mtu wa Tofauti kwa kufanya mambo ya kawaida. Ukitaka kuwa tofauti ni lazima ufanye mambo ya tofauti. Kila mmoja anatamani kuwa tofauti ila ni wachache wamefanikiwa kwa sababu “Utofauti” ni matokeo ya mchakato unaoongozwa na kanuni. Cha kwanza unachohitaji ni maarifa ya kuzielewa kanuni na cha pili ni nidhamu na utayari wa kuziishi.
Kitabu hiki ni maalumu kwaajili ya kukusaidia kwenye kuhama kutoka kwenye kundi la ukawaida kwenda kwenye kundi la Utofauti ambalo lina watu wachache. Kuwa mtu wa kawaida hakuhitaji ridhaa yako. Wala hakuna gharama yoyote unayopaswa kulipa.
Kama hujafanya maamuzi ya kuwa tofauti basi moja kwa moja unakuwa kawaida.
Customer reviews
★★★★★
Moringe L., 2 Dec, 2024
Actually I have tried to read the book but I got more than I desired