Makosa 4 Wanayofanya Waandishi Wanapotangaza Vitabu Vyao

Kwa waandishi wengi, kuuza vitabu ni kazi ngumu kuliko kuandika. Kujifunza kutangaza na kuuza kitabu ndiyo msingi wa mafanikio kwa muandishi yeyote yule. Tumekuandikia makosa 4 ambayo waandishi wengi wanafanya wanapotangaza vitabu vyao na wanajikuta mauzo yao ya vitabu yapo chini.
1. Kutangaza kitabu chako kwa kila mtu.
Lazima ujue
kitabu chako ni mahsusi kwa kundi lipi la wasomaji ili juhudi zako za kutangaza iweze kuzaa matunda.
Tunapowauliza waandishi, umeandika kitabu chako kwa kundi
lipi la wasomaji?, wengi hujibu “nimewalenga vijana zaidi” lakini kwa bahati
mbaya jibu kama hili linaonyesha udhaifu katika namna mbili; mosi, si kila
kijana atasoma kitabu chako, hivyo unakuwa na mategemeo yasiyo halisi, pili,
utapoteza muda na fedha yako kutangaza kitabu chako kwa kundi la watu wasio
sahihi wasioweza kununua.
Kutangaza kitabu ni kuwaambia kundi la wasomaji wako uliowalenga
kusoma kitabu chako. Fikiria mapema kuhusu wasomaji uliowalenga kusoma kitabu
chako hata kabla ya kumaliza kuandika kitabu
2. Huna orodha ya baruapepe za wasomaji wako.
Kutangaza kitabu chako kwa kuwatumia baruapepe wasomaji wako ni njia isiyo na gharama na huleta matokeo chanya. Tunashangazwa mno na waandishi wengi ambao
bado hawana orodha ya baruapepe ya wasomaji wao.
Kama huna orodha hii, mahali pa kuanzia ni kuwa na blogi
yako kama muandishi ambayo itakusaidia kukusanya baruapepe za wasomaji, kisha
fungua akaunti ya mailer au mailchip kutuma jumbe zako kwa wasomaji.
3. Unajitengenezea jalada la kitabu mwenyewe.
Wasomaji hawanunui vitabu ambavyo jalada lake halivutii na linaonekana ni kama
mtu alikuwa akijifunza au akijaribu. DL Bookstore tumewasaidia
waandishi wengi kupata jalada la kitabu lenye muonekano bora na linaloongeza
mauzo ya kitabu chako. Wasiliana nasi tukusaide na wewe
Pia unaweza kusoma: Maswali 5 ya kujiuliza kama jalada la kitabu linafaa
4. Unaona huwezi kutoa kitabu chako BURE au kutoa ofa ya punguzo la bei.
Baada ya miezi mitatu, kuwa na siku 5 za kuuza kitabu chako
kwa punguzo au wape wasomaji wako bure. Angalizo hapa; ni wasomaji walio kwenye
orodha yako ya baruapepe tu!.
Kutoa ofa kwa wasomaji wako huongeza idadi ya wasomaji wapya
watakaojua kazi zako na wataweza kununua vitabu vingine ulivyoandika. Ofa ni
sehemu ya kuwa karibu zaidi na wasomaji wako na watajua kuwa unawajali.
Nunua kitabu cha kusoma mwezi huu Huduma zetu kwa waandishi