Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Books
  • Publish
  • Sell
  • Courses
  • Blog
  • Support

JINSI YA KUANDIKA ‘KUHUSU KITABU’ INAYONASA WASOMAJI WASOME KITABU CHAKO

November 23, 2020 at 1:31 pm,


Kama msomaji wa vitabu, ni jambo gani la kwanza huwa unaangalia kwenye kitabu baada ya kuona jalada la kitabu? Iwe upo kwenye duka la vitabu au unanunua kitabu mtandaoni, utaangalia kuhusu kitabu – maelezo yanayohusu kitabu. Kama muandishi wa kitabu ni lazima ujue kuandika kuhusu kitabu ambayo itamnasa msomaji asome kitabu chako. Kama ulikuwa hujui, hakuna kitu kinachouza kitabu chako kama kuhusu kitabu iliyoandikwa vizuri.


Maelezo ya kuhusu kitabu siyo ufupisho wa nusu kurasa wa kitabu chako, la! Ni tangazo lako la kumfanya msomaji anunue kitabu. Kwahiyo inabidi ufikirie kuanzia  sasa kuhusu kitabu kama nyenzo ya wewe kuuza kitabu. Kuna mambo 4 ya kuzingatia unapoandika kuhusu kitabu;

1. Iwe fupi. 

Wastani wa maneno unaofaa unapoandika kuhusu kitabu ni maneno 150 mpaka 250 tu, na kwa nadra sana, yakizidi, basi yawe maneno 300. Usiwachoshe wasomaji kusoma maelezo marefu yasiyoongeza kitu.

2. Andika katika nafsi ya tatu. 

Hata kama kitabu chako umeandika katika nafsi ya kwanza, unapoandika kitabu tumia nafsi ya tatu. Mfano, “alikimbia sana lakini mbio zake hazikufua dafu, lile joka kubwa jeusi lilimfikia na…”

Get a Free PDF

Enter your email to get a free PDF "Hatua 6 rahisi za kuandika kitabu"

Thank you!

Go to your email inbox to download your free PDF

.

Pia unaweza kusoma: MAKOSA 4 WANAYOFANYA WAANDISHI WANAPOTANGAZA VITABU VYAO

3. Iwe chambo. 

Weka ujuzi wako, sentensi ya kwanza tu imnase msomaji. Usiweke blah blah zisizo na maana kwani msomaji hatanaswa kusoma zaidi na kisha kununua kitabu chako. Kuhusu kitabu ni tangazo!

4. Usitumie maneno magumu. 

Unapoandika kuhusu kitabu, tumia maneno marahisi, yenye maana ya moja kwa moja na siyo kumfanya msomaji awe kama anazunguka mbuyu kutafuta maana ya maneno. Lengo ni kuuza kitabu siyo kuonyesha ujuzi wa maneno. 


Tunatoa OFA kwa siku ya leo. Utapata kitabu cha CHOCHEA KIPAJI CHAKO kwa 3999 TZS badala ya 5000 TZS. 
Nunua sasa au weka oda kulipa baadaye. Ukiweka oda tumia kuponi SOMA. 
NUNUA    WEKA ODA    






Recent Posts

  • Mapitio ya Kitabu: Mimi Ashraf — Riwaya Inayokupeleka Ndani ya Nafsi ya Mwanadamu
    3 Jun, 2026
  • Vitabu 6 Bora vya Uwekezaji na Uhuru wa Kifedha kwa Kiswahili
    20 May, 2026
  • Vitabu Bora vya Biashara Kwa Kiswahili PDF
    18 May, 2026
  • Nukuu 24 Bora kutoka kitabu cha Hisa, Hatifungani, Vipande
    8 Apr, 2026
  • Book review: Hisa, Hatifungani, Vipande - Uwekezaji kwa Ukuaji wa Mtaji na Kipato Endelevu
    6 Apr, 2026
  • Siku ya Wanawake: Sherehekea Siku Yako na Maarifa
    7 Mar, 2026
  • Unahitaji nini ili uuza kitabu chako dlbookstore.com
    2 Mar, 2026

Categories

  • Book Recommendations
  • Book Reviews
  • Help & Support
  • Offers and discounts
  • Reading Habits & Tips
  • Writing, Publishing & Author Support

Start selling your book or course on our website — reach more readers

You will enjoy high book visibility, get paid on time and receive a monthly sales report straight to your inbox.

Start selling →

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Books
  • Return policy
  • About us
  • Publish
  • Sell
  • Blog
  • Support
DL Bookstore © 2026. All rights reserved | Made with ❤️ in Tanzania.