Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support

Njia Nne Za Kumsaidia Muandishi Kuongeza Orodha Ya Imeli [Baruapepe) Za Wasomaji Wake.

May 21, 2021 at 12:35 pm,


Imeli (Baruapepe) ni njia mojawapo kwa muandishi kuwasiliana na wasomaji wake wanaofuatilia kazi zake kama kitabu kipya kinachotoka, ofa mbalimbali na n.k. Kutumia imeli kunamleta karibu zaidi muandishi na watu wanaopenda kazi zake pengine kuliko njia nyingine kwa sababu ujumbe huenda moja kwa moja kwenye kikasha (inbox) cha muandishi ama kwa msomaji.


Tumekuandalia njia tano ambazo muandishi anaweza kutumia kuongea orodha ya Imeli za wasomaji wake;

1. Tengeneza sumaku ya kumnasa msomaji. Hii ndiyo njia iliyozoeleka zaidi na ina matokeo makubwa mno. Kutengeneza sumaku inamaanisha muandishi anatakiwa ampe kitu mfano ofa ya kitabu bure ili msomaji wake ampe imeli yake ambayo atatumiwa kitabu huko. Mfano, sumaku ya mwandishi inaweza kusomeka “Weka baruapepe yako hapa chini kupakua kitabu changu bure” na msomaji ataweka hapo baruapepe yake ya kupokelea hicho kitabu. Ukiacha kitabu cha bure, msomaji atafaidika na ofa mbalimbali za vitabu vyako, kupata taarifa ya mapema ya kitabu unachotaka kutoa na n.k

Get a Free Ebook

Enter your email to download a free ebook: Hatua 6 za Kuandika Kitabu 

Thank you!

You have successfully joined our subscriber list.

.

2. Tumia tovuti yako. Muandishi wa kitabu lazima awe na tovuti. Kwenye tovuti yako weka fomu ya kujiandikisha (sign up form) ambayo wasomaji wako wataweka imeli zao ili kupokea machapisho unayoweka kwenye blogi yako, taarifa za kozi za mtandaoni unazotoa na n.k. Msomaji anapotembelea tovuti yako anaweza kuvutika kutaka kufatilia zaidi mambo unayoweka kwenye hiyo tovuti na njia pekee ya kuunganika naye ni kupitia imeli yake. Hakikisha ile fomu ya kujiandikisha umeiweka juu ya tovuti (header) ama chini ya tovuti (footer) na inaonekana vizuri

3. Tumia sehemu ya nyuma ya kitabu (backmatter). Usimuache hewani msomaji wako anapomaliza kusoma kitabu chako, mwekee kiunganishi (link) ya kuweka imeli yake ili aendelee kukufatilia zaidi. Njia hii hufaa sana kwa waandishi wanaotoa vitabu vyao kama ebook ijapokuwa hata kwa nakala ngumu unaweza kuitumia lakini inaweza kuwa na matokeo kiduchu.

4. Tumia mitandao ya kijamii. Kama muandishi ana ukurasa wa Facebook au akaunti ya Instagram na Twitter basi anaweza kuweka na kiunganishi ambacho kitawapeleka wasomaji wake mahali pa kuweka imeli zao.

Sasa umeshapata imeli za kutosha za wasomaji wako nini kinafuata? Endelea kuwapa ofa zako, machapisho yako na masasisho yako mbalimbali. Jambo la kuzingatia ni hili, usitume imeli nyingi mno kwa wiki, angalau imeli mbili mpaka nne kwa wiki zinatosha. Kuna baadhi ya wasomaji wako wanaweza kujiondoa kwenye orodha yako na hilo lisikupe shaka; huwa ni jambo la kawaida.

Soma makala nyingine

  1. HATUA TANO ZA KUWATAMBUA WASOMAJI WAKO WALENGWA
  2. NJIA MBILI MUHIMU ZA KUUZA KITABU KWA MASHABIKI WAKO
  3. Tabia 5 zinazoleta mafanikio kwa muandishi


100% Free courses

Enter your email below and be the first to get our updates about new courses

Thank you!

You have successfully joined our subscriber list.

.




Recent Posts

  • Umechoka na Minyama Uzembe? Suluhisho la Kupungua Uzito Limepatikana!
    17 Apr, 2025
  • Vitabu Bora vya Pasaka vya Kukuimarisha Kiroho – Vinapatikana Sasa DL Bookstore
    11 Apr, 2025
  • 4 Benefits of Selling Your Book Through DL Bookstore
    20 Mar, 2025
  • Download Entrepreneurship Books (PDF) in Swahili
    10 Feb, 2025
  • Download Nine (9) Must-Read Books for Girls and Women 📚✨
    4 Feb, 2025
  • A Tanzanian Platform for Selling Books Online
    4 Feb, 2025
  • Jinsi ya Kuandika Caption Inayochochea Mauzo ya Kitabu Chako
    23 Nov, 2024

selling_book-1.png

Enroll in 100% free courses

100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

Start learning →

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2025. All rights reserved.