Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Agano Lililo Bora
“Ishinde vita ya madhabahu za siri kwa njia nyepesi”
Vita vya kimadhabahu vimewaangusha, kuwafukuza na hata kuwaua watumishi wengi wa Mungu
Je! Unaona ugumu katika kumtumikia Mungu mahali ulipo mpaka unatamani kuacha huduma na kuhamia eneo lingine, wakati unajua kabisa ndani yako kuna wito wa kumtumikia Mungu?
Unatamani kupata matokeo mazuri katika kila unalolifanya, lakini kinachokuja kwako sicho ulichotarajia, na kwa kadiri unavyopambana kujinasua unaona kama milango yote imefungwa na hujui nani anayefunga.
Unaona upinzani mkubwa sana katika huduma, ndoa, familia, kazini kwako na hujui wapi upinzani unatokea na hujui namna gani upinzani huo utakwisha ili uwe huru?. Kitabu hiki cha Agano Lililo Bora kitakuwa msaada kwako katika kujua ni nini kipo nyuma ya hayo na utapataje unayoyatarajia katika huduma, afya, elimu, uchumi, ndoa na familia.
Kisome kitabu hiki mpaka mwisho.