Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Books
  • Publish
  • Sell
  • Courses
  • Blog
  • Support

Riwaya 5 zinazobamba

September 9, 2020 at 12:47 pm,


Kama wewe ni mlevi wa riwaya, basi tunakuletea riwaya tatu zinazobamba vilivyo kwa wasomaji. Tumekuwekea maelezo mafupi ya kila riwaya kukuonjesha ndani yake kuna nini. Twende pamoja sasa;


1. FUNGATE

“Noella, unanipa mtihani mgumu mno maishani mwangu,” Tony alimwambia Noella.

Noella alimtazama Tony. Machozi yalimtiririka mithili ya bomba la maji. Hakuwa tayari kukubaliana na ukweli kuwa Tony, sasa si sehemu ya maisha yake tena.

Noella yumo hotelini kwenye fungate. Ni saa chache tu baada ya harusi yao. Yeye na mumewe, Justine, wamemaliza kupata amshakinywa ndani ya mgahawa uliomo hotelini humo.

Mara, Noella anamwona Tony. Mpenzi wake wa zamani. Tony, ndiye mwanaume aliyewahi kumpenda kupindukia. Leo, tena akiwa kwenye fungate, anamwona.

Hii ni baada ya kutomwona kwa zaidi ya miaka minne. Tena, akiamini Tony alikwishafariki.

Je, kiapo alichokitoa madhabahuni, kuwa kifo pekee ndicho kitakachomtenganisha na Justine, kitazishinda hisia zake juu ya Tony?”

Fungate - Fasihi - Buy books - We have the best and affordable books (dlbookstore.com)

2.  NITAIAMBIA NINI FAMILIA YANGU

“Waliitwa na daktari kupokea majibu yao. Daktari aliwauliza "mpo tayari kupokea majibu yenu mbele ya mashahidi wenu? na kila mmoja yuko tayari kusikia majibu ya mwenzake?".  Joseph na Irene waliitikia kwa pamoja wakasema "ndiyo daktari". Daktari akaanza kwa kusema "UKIMWI ni ugonjwa wa kawaida sana, ukiwa na Ukimwi na ukafuata masharti ya daktari unaweza kuishi miaka mingi. Hivyo basi baada ya majibu haya ukiwa una virusi vya UKIMWI au hauna, lazima uwe makini na maisha yako ya kila siku. Kama huna virusi vya UKIMWI inakupasa uwe makini ili usiweze kupata virusi hivyo, pia kama una Ukimwi uepuke ngono zembe ili usieneze kwa wengine. Pia wanandoa wanaweza kuishi pamoja, mmoja akiwa na virusi vya Ukimwi na mwingine hana ikiwa tu watafuata ushauri wa daktari na wakapata mtoto asiye na maambukizi". Kisha Daktari akatoa hitimisho kwa kusema "nimewapima kwa makini na majibu ni kama ifuatavyo "Benard huna maambukizi ya virusi vya UKIMWI hongera sana, ila kwa bahati mbaya Irene una maambukizi ya virusi vya ukimwi, lakini usikate tamaa bado una nafasi ya kuishi kama nilivyotangulia kusema hapo mwanzo"

Nitaiambia nini familia yangu - Fasihi - Buy books - We have the best and affordable books (dlbookstore.com)

3.   MHESHIMIWA THE DON 

“Mabrook alimaarufu The Don ni mtu mwenye jina kubwa sana nchini. Kwanza kwa sababu ni miongoni kwa mawaziri wachapakazi na anayekubalika sana kwa wananchi wa rika zote lakini pia ni mtu wa watu anayetoa misaada mingi wa raia. Ni kiongozi anayepewa nafasi kubwa ya kushika madaraka ya juu zaidi nchini.

Pamoja na hayo, Mheshimiwa Mabroo si mtu wa kawaida kwa kila hali. Akihusishwa na ushirikina unaosababisha mauaji ya kutisha ya albino, viungo vya binadamu na mauaji ya watu maarufu.

Kisasi cha mapenzi kinaibua maozo yote ya Mheshimiwa The Don. Machera ni mpelelezi makini anayeibua huo kwa kushirikiana na mwanaharakati wa haki za binadamu Maisha Nchagwa

Mheshimiwa the Don - Fasihi - Buy books - We have the best and affordable books (dlbookstore.com)

4. JIPU NDANI YA UBONGO

Naanza kuumwa nikidhani ni ugonjwa wa kawaida. Hospitali pia natibiwa magonjwa ya kawaida; Malaria, homa ya tumbo na maambukizi ya bakteria. Wiki tatu zinapita, nazidi kuumwa, kichwa, kutapika na mwili kuisha nguvu. Najaribu hospitali nyingine na kugundulika kuwa nina uvimbe. Ndio, uvimbe kwenye ubongo. Nauita JIPU, kwani umeshikamana na ubongo kama doa lilivyo kwenye nguo. Natakiwa kufanyiwa upasuaji wa haraka vinginevyo nitakufa ghafla. Daktari anamwambia mume wangu akubaliane na hatari iliyoko mbele yangu ya kupoteza kuona, kupooza, kupoteza kumbukumbu au kufa baada ya upasuaji. Godfrey, mume wangu, analazimika kufanya maamuzi yenye hatari kubwa kwa maisha yangu.

Nafsini namuamini Mungu kuwa HAKUNA KITAKACHOPUNGUA, HAKUNA KITAKACHOVUNJIKA.

Hii siyo hadithi, ni simulizi la kweli. Leo ni mwaka mmoja umepita, na mimi mwenyewe nimeandika kitabu hiki, kuelezea ukuu wa Mungu awezaye kufufua hata waliokufa, jinsi alivyotenda kwangu.

Jipu ndani ya ubongo - Simulizi ya kweli - Fasihi - Buy books - We have the best and affordable books (dlbookstore.com)

5. KUSANYA VIPANDE VYAKE

Kusanya Vipande Vyake ni hadithi nzuri ya kiswahili inayomuhusu binti mmoja anaye julikana kwa jina la Furaha. Ni binti mkorofi, jeuri, kisirani, na mwenye chuki na dharau nyingi sana. Hakuna mtu anaye mpenda, na pia hajali watu wakimchukia, yupo na maisha yake binafsi ambayo watu wengi hua hawamuelewi. Ni hadithi nzuri sana na ya kusisimu, itakayo kupa funzo kubwa maishani, na kukufanya uweze kuyatazama maisha kwa jicho la tofauti, na uanze kichukua tahadhari ambazo pengine umekua ukizipuuzia. Fuatana nami hadi mwisho wa hadithi hii tamu, na ya kusisimua, tukajifunze vitu kupitia maisha ya Furaha

Kusanya vipande vyake - Fasihi - Buy books - We have the best and affordable books (dlbookstore.com)




Recent Posts

  • Siku ya Wanawake: Sherehekea Siku Yako na Maarifa
    7 Mar, 2026
  • Unahitaji nini ili uuza kitabu chako dlbookstore.com
    2 Mar, 2026
  • Kijana anasoma vitabu kama hivi (Download vitabu 10 hapa)
    13 Jan, 2026
  • Vitabu Nane (8) vya Elimu ya Fedha - PDF Download
    21 Dec, 2025
  • Tumia mbinu hizi rahisi na uwe miongoni mwa 1% wanaomaliza kusoma vitabu
    5 Dec, 2025
  • Faida za Kuhariri Kitabu kwa Waandishi na Njia za Kukamilisha Uhariri
    1 Dec, 2025
  • Ukitumia njia hizi, utapenda kusoma vitabu
    27 Nov, 2025

Categories

  • Book Recommendations
  • Book Reviews
  • Help & Support
  • Offers and discounts
  • Reading Habits & Tips
  • Writing, Publishing & Author Support

Start selling your book or course on our website — reach more readers

You will enjoy high book visibility, get paid on time and receive a monthly sales report straight to your inbox.

Start selling →

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Books
  • About us
  • Publish
  • Sell
  • Blog
  • Support
DL Bookstore © 2026. All rights reserved.