Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support

MAMBO 3 YA KUZINGATIA KUPATA JINA LA KITABU LINALOUZA SANA.

May 25, 2021 at 3:05 pm,

Jina zuri la kitabu lina uwezo wa kumnasa msomaji akataka kujua zaidi maudhui ya kitabu chako. Jina la kitabu ni maneno machache tu lakini linaweza kuwa ndoano ya kuwanasa wasomaji na ukauza nakala nyingi za kitabu chako.


Kama una imeli za wasomaji wako, unaweza anza kuwadodosa kuhusu jina la kitabu unachotaka kukitoa kwa kuwatumia rasimu kadhaa za majina uliyoandika kisha utapata majibu ya kila msomaji wako na utamalizia na zoezi la kupembua maoni yao na kuyafanyia kazi.

Mbinu nyingine inayofanya kazi na itakuletea matokeo bora sana ni kuandika majina kadhaa unayofikiria kwamba yatafaa kubeba jina la kitabu. Ukimaliza kuandika haya majina sasa yaache ili akili yako ipate muda wa kupumua , kuchakata na kumeng’enya kila jina la kitabu uliloandika. Unaweza endelea na mambo mengine kama kusoma vitabu vingine, tembea tembea ama sikiliza muziki. Baadaye sasa, rudia kusoma hayo majina ya kitabu na utashangaa unaibuka na jina la kitabu lilio zuri na bora.

Get a Free Ebook

Enter your email to download a free ebook: Hatua 6 za Kuandika Kitabu 

Thank you!

You have successfully joined our subscriber list.

.

Jambo la kuzingatia katika unapochagua, kuandika majina kadhaa unayoona yanafaa na kisha kurudia kuchagua tena ni uzingatiaji wa aina ya kitabu unachoandika. Chagua jina la kitabu kulingana na aina ya kitabu, mfano; kama kitabu chako ni riwaya ya taharuki au riwaya ya mapenzi ama ni kitabu cha biashara au cha kiroho, basi jina la kitabu liendane na aina hiyo.

Unapoandika na kuchagua jina la kitabu litakalouza sana, basi zingatia mambo haya rahisi na utapata matokeo bora;

1. Tumia kanuni ya K.I.S.S. Kirefu cha K.I.S.S ni Keep It Simple, Smarty ikimaanisha kuwa weka iwe rahisi na inayoeleweka. Kwa kutumia kanuni hii ya K.I.S.S, andika jina la kitabu lililo fupi, rahisi na linaloeleweka. Usifanye msomaji kujitafutia maana yake tofauti na yako ulokusudia. Usiandike jina la kitabu refu. Inakubalika kabisa kwamba walau jina la kitabu lisizidi maneno matano. Kama refu sana, basi fikiria kutumia “subtitle”.

2. Chora picha. Jina zuri na linalouza sana la kitabu ni lile ambalo msomaji akisoma atatengeneza picha fulani hivi kwenye akili yake. Unapoandika na kuchagua majina kadhaa uliyoandika, zingatia hili, kwamba jina la kitabu liweze kutengeneza ama kuchora picha. Tumia maneno ama lugha ambayo itamfikirisha msomaji atake kujua zaidi.

100% Free courses

Enter your email below and be the first to get our updates about new courses

Thank you!

You have successfully joined our subscriber list.

.

3. Liwe na upekee. Fanya “homework” yako kujua kama jina unalotaka kulitumia kwenye kitabu chako lilishatumiwa tayari au bado. Kusiwe na ufanano na jina la kitabu ambalo tayari kitabu chake kipo sokoni. Kitabu chako kiwe na jina lenye upekee fulani ili wasomaji wako wasichanganye na vitabu vingine.

Jina la kitabu linalouza huvutia aina ya wasomaji ambao ni walengwa wa kitabu chako. Ili kuwa na matokeo bora zaidi, jina zuri la kitabu likae kwenye jalada la kitabu lililosanifiwa vizuri. Ikiwa ungetaka jalada zuri la kitabu, angalia vifurushi vyetu mbalimbali kuendana na bajeti yako.

Tuandikie maoni yako hapa chini. Karibu!.

Soma makala nyingine

1. Hatua Tano Za Kuwatambua Wasomaji Wako Walengwa

2. Njia Mbili Muhimu Za Kuuza Kitabu Kwa Mashabiki Wako

3. Tabia 5 Zinazoleta Mafanikio Kwa Muandishi

4. Njia Nne Za Kumsaidia Muandishi Kuongeza Orodha Ya Imeli[Baruapepe) Za Wasomaji Wake



Recent Posts

  • Umechoka na Minyama Uzembe? Suluhisho la Kupungua Uzito Limepatikana!
    17 Apr, 2025
  • Vitabu Bora vya Pasaka vya Kukuimarisha Kiroho – Vinapatikana Sasa DL Bookstore
    11 Apr, 2025
  • 4 Benefits of Selling Your Book Through DL Bookstore
    20 Mar, 2025
  • Download Entrepreneurship Books (PDF) in Swahili
    10 Feb, 2025
  • Download Nine (9) Must-Read Books for Girls and Women 📚✨
    4 Feb, 2025
  • A Tanzanian Platform for Selling Books Online
    4 Feb, 2025
  • Jinsi ya Kuandika Caption Inayochochea Mauzo ya Kitabu Chako
    23 Nov, 2024

selling_book-1.png

Enroll in 100% free courses

100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

Start learning →

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2025. All rights reserved.